Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 20:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 “Usisahau kuiweka takatifu siku ya Sabato.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 “Usisahau kuiweka takatifu siku ya Sabato.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 “Usisahau kuiweka takatifu siku ya Sabato.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Ikumbuke siku ya Sabato, uitakase.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Ikumbuke siku ya Sabato, uitakase.

Tazama sura Nakili




Kutoka 20:8
22 Marejeleo ya Msalaba  

Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.


Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.


Siku hizo niliona katika Yuda watu wengine waliosindika zabibu ili kupata mvinyo siku ya sabato, na wengine waliochukua miganda, na kuwapakia punda zao; tena na mvinyo, na zabibu, na tini, na namna zote za mizigo, waliyoileta Yerusalemu, siku ya sabato; nami nikashuhudia juu yao siku ile waliyouza vyakula.


ukawajulisha sabato yako takatifu, na ukawapa maagizo, na amri, na sheria, kwa mkono wa mtumishi wako, Musa.


Siku sita utafanya kazi yako, na siku ya saba utapumzika; ili kwamba ng'ombe wako na punda wako wapate kupumzika, kisha mwana wa mjakazi wako na mgeni wapate kuburudika.


BWANA akasema na Musa, na kumwambia,


Musa akakutanisha mkutano wote wa wana wa Israeli, na kuwaambia, Maneno aliyoyausia BWANA ni haya, kwamba myafanye.


Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wowote.


Kama ukigeuza mguu wako usiivunje sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe;


BWANA asema hivi, Jihadharini nafsi zenu, msichukue mzigo wowote siku ya sabato, wala msiulete ndani kwa malango ya Yerusalemu;


wala msitoe mzigo katika nyumba zenu siku ya sabato, wala msifanye kazi yoyote; bali itakaseni siku ya sabato, kama nilivyowaamuru baba zenu;


Na itakuwa, kama mkinisikiliza mimi kwa bidii, asema BWANA, msiingize mzigo wowote katika mlango wa mji huu siku ya sabato, bali muitakase siku ya sabato, bila kufanya kazi yoyote siku hiyo;


zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.


Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.


Zishikeni Sabato zangu, mpaheshimu patakatifu pangu; mimi ndimi BWANA.


Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yoyote; ni Sabato kwa BWANA katika makao yenu yote.


Zishikeni Sabato zangu, na kupastahi patakatifu pangu; mimi ndimi BWANA.


Kisha wakati huo wana wa Israeli walipokuwako jangwani, wakamwona mtu mmoja akikusanya kuni siku ya Sabato.


Ishike siku ya Sabato uitakase, kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo