Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 17:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Akapaita mahali pale jina lake Masa, na Meriba kwa sababu ya ugomvi wa wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu BWANA, wakisema, Je! BWANA yu kati yetu au sivyo?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mahali hapo Mose akapaita “Masa” na “Meriba”, kwa sababu Waisraeli walimnungunikia na kumjaribu Mwenyezi-Mungu wakisema, “Je, kweli Mwenyezi-Mungu yu pamoja nasi?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mahali hapo Mose akapaita “Masa” na “Meriba”, kwa sababu Waisraeli walimnungunikia na kumjaribu Mwenyezi-Mungu wakisema, “Je, kweli Mwenyezi-Mungu yu pamoja nasi?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mahali hapo Mose akapaita “Masa” na “Meriba”, kwa sababu Waisraeli walimnung'unikia na kumjaribu Mwenyezi-Mungu wakisema, “Je, kweli Mwenyezi-Mungu yu pamoja nasi?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Naye akapaita mahali pale Masa na Meriba, kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu Mwenyezi Mungu wakisema, “Je, Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi au la?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Naye akapaita mahali pale Masa, na Meriba kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu bwana wakisema, “Je, bwana yu pamoja nasi au la?”

Tazama sura Nakili




Kutoka 17:7
21 Marejeleo ya Msalaba  

Wakamghadhabisha penye maji ya Meriba, Hasara ikampata Musa kwa ajili yao,


Wakamjaribu Mungu mioyoni mwao Kwa kutaka chakula kwa tamaa zao.


Katika shida uliniita nikakuokoa; Nilikuitikia kutoka maficho yangu ya radi; Nilikujaribu penye maji ya Meriba.


Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya, Ee Israeli, kama ukitaka kunisikiliza;


Msifanye mioyo yenu kuwa migumu; Kama ilivyokuwa huko Meriba Kama siku ile katika Masa jangwani.


Kwa hiyo hao watu wakamgombeza Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwa nini mnanigombeza? Mbona mnamjaribu BWANA?


Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.


Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.


Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea BWANA, na kusema, Je! Hayupo BWANA katikati yetu? Hapana neno baya lolote litakalotufikia.


kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu;


Maji haya ni maji ya Meriba; kwa sababu wana wa Israeli waliteta na BWANA, naye alijionesha kuwa mtakatifu kati yao.


Haruni atakusanywa awe pamoja na watu wake; kwa kuwa hataingia katika nchi niliyowapa wana wa Israeli, kwa sababu mliasi kinyume cha neno langu hapo penye maji ya Meriba.


kwa sababu mliasi juu ya neno langu katika jangwa la Sini wakati wa mateto ya mkutano, wala hamkunistahi, hapo majini, mbele ya macho yao. (Maji hayo ndiyo maji ya Meriba ya Kadeshi katika jangwa la Sini.)


Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.


Ndipo hasira yangu itakapowaka juu yao siku hiyo, nami nitawaacha, nitawaficha uso wangu, nao wataliwa, tena watajiliwa na mambo maovu mengi na mashaka; hata waseme siku hiyo, Je! Kujiliwa kwetu na maovu haya si kwa sababu Mungu wetu hayumo kati yetu?


Akamnena Lawi, Thumimu yako na Urimu yako vina mtakatifu wako, Uliyemjaribu huko Masa; Ukateta naye kwenye maji ya Meriba.


Msimjaribu BWANA, Mungu wenu, kama mlivyomjaribu huko Masa.


Tena huko Tabera, na Masa, na Kibroth-hataava mlimtia BWANA hasira.


Naye Finehasi, mwana wa Eleazari, kuhani, akawaambia wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na wana wa Manase, akasema, Siku hii ya leo tumejua ya kwamba BWANA yu kati yetu, kwa sababu hamkukosa katika jambo hili mbele ya BWANA; sasa ninyi mmewaokoa wana wa Israeli na mkono wa BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo