Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 16:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

28 BWANA akamwambia Musa, Mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Hapo Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Mpaka lini mtakataa kuzitii amri na Sheria zangu?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Hapo Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Mpaka lini mtakataa kuzitii amri na Sheria zangu?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Hapo Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Mpaka lini mtakataa kuzitii amri na Sheria zangu?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Je, mtaacha kushika maagizo na maelekezo yangu hadi lini?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Ndipo bwana akamwambia Musa, “Je, mtaacha kushika maagizo na maelekezo yangu mpaka lini?

Tazama sura Nakili




Kutoka 16:28
19 Marejeleo ya Msalaba  

Walakini hawakutaka kusikia, bali walifanya shingo zao kuwa ngumu, kama shingo za baba zao, wasiomwamini BWANA, Mungu wao.


Wakazikataa sheria zake, na agano lake, alilolifanya na baba zao; na shuhuda zake alizowashuhudia; wakafuata ubatili, wakawa ubatili, nao wakaandamana na mataifa waliowazunguka, ambao BWANA alikuwa amewaagiza, wasitende kwa mfano wao.


Lakini punde wakayasahau matendo yake, Wakakosa kungojea ushauri wake.


Hawakulishika agano la Mungu; Wakakataa kufuata sheria yake;


Kwa kuwa hawakumwamini Mungu, Wala hawakuutumainia wokovu wake.


Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie.


Ikawa siku ya saba wengine wakatoka kwenda kukiokota, wasikione.


Angalieni, kwa kuwa BWANA amewapa ninyi hiyo Sabato, kwa sababu hii huwapa siku ya sita chakula cha siku mbili; kaeni kila mtu mahali pake, mtu awaye yote asiondoke mahali pake kwa siku ya saba.


Naye akasema, Sikilizeni sasa, enyi nyumba ya Daudi; Je! Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia?


tena kichwa cha Efraimu ni Samaria, na kichwa cha Samaria ni mwana wa Remalia. Ikiwa hamtasimama imara katika imani, hamtathibitika kamwe.


Ee Yerusalemu, jioshe moyo wako usiwe na uovu, upate kuokoka. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako hata lini?


Makao yako ya katikati ya hadaa; kwa hadaa wanakataa kunijua mimi, asema BWANA.


Lakini nyumba ya Israeli waliniasi jangwani; hawakuenda katika amri zangu, wakazikataa hukumu zangu, ambazo mwanadamu ataishi kwazo, kama akizitenda; na sabato zangu walizitia unajisi sana; ndipo nikasema, Nitamwaga hasira yangu juu yao jangwani, ili niwaangamize.


kwa sababu walizikataa hukumu zangu, wala hawakuenda katika amri zangu, wakazitia unajisi sabato zangu, kwa maana mioyo yao iliandama vinyago vyao.


Nao umeasi amri zangu, kwa kutenda mabaya kuliko mataifa hayo, nao umeasi sheria kuliko nchi hizo ziuzungukazo; maana wamezikataa hukumu zangu, wala hawakuenda katika sheria zangu.


BWANA akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hadi lini? Wasiniamini hadi lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao.


BWANA akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa.


Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hadi lini? Nichukuliane nanyi hadi lini? Mleteni kwangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo