Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 16:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Neno hili ndilo aliloagiza BWANA, Okoteni ninyi kitu hicho kila mtu kama ulaji wake ulivyo; kila mtu pishi moja kama hesabu ya watu wenu ilivyo; ndivyo mtakavyotwaa, kila mtu kwa ajili ya hao walioko hemani mwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Mwenyezi-Mungu ameamuru mfanye hivi: Kila mtu na akusanye chakula kiasi anachoweza kula; ataokota kiasi cha pishi moja kwa kila mtu hemani mwake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Mwenyezi-Mungu ameamuru mfanye hivi: Kila mtu na akusanye chakula kiasi anachoweza kula; ataokota kiasi cha pishi moja kwa kila mtu hemani mwake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Mwenyezi-Mungu ameamuru mfanye hivi: kila mtu na akusanye chakula kiasi anachoweza kula; ataokota kiasi cha pishi moja kwa kila mtu hemani mwake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu ameamuru: ‘Kila mmoja akusanye kiasi anachohitaji. Chukueni pishi moja kwa kila mtu mliye naye katika hema lenu.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Hivi ndivyo bwana alivyoamuru: ‘Kila mmoja akusanye kiasi anachohitaji. Chukueni pishi moja kwa kila mtu mliye naye katika hema yenu.’ ”

Tazama sura Nakili




Kutoka 16:16
4 Marejeleo ya Msalaba  

Wana wa Israeli wakafanya hivyo, wakaokota wengine zaidi, wengine kupungua.


Nao walipoipima kwa pishi, yeye aliyekuwa ameokota kingi hakubakiwa na kitu, na yeye aliyekuwa ameokota kichache hakupungukiwa; wakaokota kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa.


Hiyo omeri ni sehemu kumi ya efa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo