Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 15:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Adui akasema, Nitafuata, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Adui alijisemea, ‘Nitawafuata na kuwakamata; nitagawanya nyara mpaka hamu yangu iishe. Tutaufuta upanga wetu, tutawaangamiza kwa mkono wetu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Adui alijisemea, ‘Nitawafuata na kuwakamata; nitagawanya nyara mpaka hamu yangu iishe. Tutaufuta upanga wetu, tutawaangamiza kwa mkono wetu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Adui alijisemea, ‘Nitawafuata na kuwakamata; nitagawanya nyara mpaka hamu yangu iishe. Tutaufuta upanga wetu, tutawaangamiza kwa mkono wetu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Adui alijivuna, ‘Nitawafuatia, nitawapata. Nitagawanya nyara; nitajishibisha kwao. Nitafuta upanga wangu na mkono wangu utawaangamiza.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Adui alijivuna, ‘Nitawafuatia, nitawapata. Nitagawanya nyara; nitajishibisha kwa wao. Nitafuta upanga wangu na mkono wangu utawaangamiza.’

Tazama sura Nakili




Kutoka 15:9
15 Marejeleo ya Msalaba  

Benyamini ni mbwamwitu mwenye kuraruararua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka.


Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza; Wala sikurudi nyuma hadi walipokomeshwa.


Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.


Ndipo Ben-hadadi akatuma kwake, akasema, Miungu wanifanyie hivi na kuzidi, yakiwa mavumbi ya Samaria yatatosha makonzi ya watu wote walio miguuni pangu.


Mfalme wa Misri aliambiwa ya kuwa wale watu wamekwisha kimbia; na moyo wa Farao, na mioyo ya watumishi wake, iligeuzwa iwe kinyume cha hao watu, nao wakasema, Ni nini jambo hili tulilotenda, kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena?


Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.


Katika miungu yote ya nchi hizi ni nani waliookoa nchi yao kutoka kwa mkono wangu, hata BWANA auokoe Yerusalemu kutoka kwa mkono wangu?


Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawana nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.


Wakalia huko, Farao, mfalme wa Misri, ni kishindo tu; muda alioandikiwa ameuacha upite.


Ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe; Wakaja kama kisulisuli ili kunitawanya; Kama wakifurahi kuwameza maskini kwa siri.


lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang'anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.


Je! Hawakupata mateka na kuyagawanya, Kijakazi, vijakazi wawili, kwa kila mtu? Kwa Sisera nyara ya mavazi ya rangi mbalimbali, Nyara za mavazi ya rangi mbalimbali ya darizi; Ya rangi mbalimbali ya darizi, pande zote mbili, Juu ya shingo za hao mateka.


Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo