Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 15:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa kilima, Vilindi vikagandamana katikati ya bahari.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Kwa pumzi ya pua yako maji yalirundikana, mawimbi yakasimama wima kama ukuta; vilindi katikati ya bahari vikagandamana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Kwa pumzi ya pua yako maji yalirundikana, mawimbi yakasimama wima kama ukuta; vilindi katikati ya bahari vikagandamana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Kwa pumzi ya pua yako maji yalirundikana, mawimbi yakasimama wima kama ukuta; vilindi katikati ya bahari vikagandamana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Kwa pumzi ya pua yako maji yalijilundika. Mawimbi ya maji yakasimama imara kama ukuta, vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Kwa pumzi ya pua zako maji yalijilundika. Mawimbi ya maji yakasimama imara kama ukuta, vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.

Tazama sura Nakili




Kutoka 15:8
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake BWANA, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.


Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika.


Hukusanya maji ya bahari chungu chungu, Huviweka vilindi katika ghala.


Aliipasua bahari akawavusha; Aliyafanya maji yasimame kama ukuta.


Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni kuta upande wao wa kulia, na upande wao wa kushoto.


bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.


Tazama, nitatia roho ndani yake, naye atasikia uvumi, na kurudi hadi nchi yake mwenyewe, nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.


Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake.


Ukaikanyaga bahari kwa farasi wako, Chungu ya maji yenye nguvu.


Hapo ndipo atakapofunuliwa yule mwasi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa dhihirisho la kuja kwake;


Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la BWANA, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yataacha kutiririka, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama kichuguu.


ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa kichuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyoteremkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yataacha kutiririka kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo