Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 15:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 BWANA, mkono wako wa kulia umepata fahari ya uwezo, BWANA, mkono wako wa kulia wawasetaseta adui.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 “Mkono wako wa kulia ee Mwenyezi-Mungu watukuka kwa nguvu; kwa mkono wako wa kulia ee Mwenyezi-Mungu wawaponda adui.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 “Mkono wako wa kulia ee Mwenyezi-Mungu watukuka kwa nguvu; kwa mkono wako wa kulia ee Mwenyezi-Mungu wawaponda adui.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 “Mkono wako wa kulia ee Mwenyezi-Mungu watukuka kwa nguvu; kwa mkono wako wa kulia ee Mwenyezi-Mungu wawaponda adui.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Mkono wako wa kuume, Ee Mwenyezi Mungu ulitukuka kwa uweza. Mkono wako wa kuume, Ee Mwenyezi Mungu, ukamponda adui.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 “Mkono wako wa kuume, Ee bwana ulitukuka kwa uweza. Mkono wako wa kuume, Ee bwana, ukamponda adui.

Tazama sura Nakili




Kutoka 15:6
27 Marejeleo ya Msalaba  

Dhihirisha fadhili zako za ajabu Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia; Kwa mkono wako wa kulia Uwaokoe kutoka kwa adui zao.


Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.


Ni nani Mfalme wa utukufu? BWANA mwenye nguvu, hodari, BWANA hodari wa vita.


Maana hawakuitwaa nchi kwa upanga wao, Wala hawakupata ushindi kwa mkono wao; Bali mkono wako wa kulia, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa ulipendezwa nao.


Ee Mungu, Wewe ndiwe mfalme wangu, Uagize mambo ya wokovu kwa Yakobo.


Ili wapenzi wako waopolewe, Utuokoe kwa mkono wako wa kulia, utuitikie.


Mbona unaurudisha mkono wako, Naam, mkono wako wa kulia, Uutoe kifuani mwako, Ukawaangamize kabisa.


Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kulia wake Aliye Juu.


Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako, Fadhili na kweli zimo mbele za uso wako.


Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kulia, Na mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.


Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?


Ulinyosha mkono wako wa kulia, Nchi ikawameza.


Hofu na woga zimewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee BWANA, Hata watakapovuka watu wako uliowanunua.


Musa akamwambia mkwewe mambo hayo yote BWANA aliyomtenda Farao na Wamisri kwa ajili ya Israeli, na mambo mazito yote yaliyowapata njiani, na jinsi BWANA alivyowaokoa.


Nami nitaunyosha mkono wangu, na kuipiga Misri kwa ajabu zangu zote, nitakazofanya kati yake, kisha baadaye atawapa ruhusa kwenda.


BWANA akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake.


Naye atapavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, kinavyovunjwavunjwa kikatili, hata hakipatikani katika vipande vyake kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, au kuteka maji kisimani.


Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.


BWANA ameweka wazi mkono wake mtakatifu Machoni pa mataifa yote; Na ncha zote za dunia Zitauona wokovu wa Mungu wetu.


Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu, kwa mkono wa kulia wa Musa? Aliyeyatenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele?


Nitawagonganisha, mtu na mwenzake, naam, baba za watu na watoto wao pamoja, asema BWANA; sitahurumia, wala sitaachilia, wala sitarehemu, hata nisiwaangamize.


Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]


naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.


Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu dunia yote; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo