Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 13:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 BWANA naye akawatangulia mchana ndani ya wingu mfano wa nguzo, ili awaongoze njia; na usiku, ndani ya moto mfano wa nguzo, ili kuwapa nuru; wapate kusafiri mchana na usiku;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Mchana Mwenyezi-Mungu aliwatangulia katika mnara wa wingu kuwaonesha njia, na usiku aliwatangulia katika mnara wa moto kuwaangazia, ili waweze kusafiri mchana na usiku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Mchana Mwenyezi-Mungu aliwatangulia katika mnara wa wingu kuwaonesha njia, na usiku aliwatangulia katika mnara wa moto kuwaangazia, ili waweze kusafiri mchana na usiku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Mchana Mwenyezi-Mungu aliwatangulia katika mnara wa wingu kuwaonesha njia, na usiku aliwatangulia katika mnara wa moto kuwaangazia, ili waweze kusafiri mchana na usiku.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Wakati wa mchana Mwenyezi Mungu aliwatangulia kwa nguzo ya wingu kuwaongoza katika njia yao, na wakati wa usiku aliwatangulia kwa nguzo ya moto kuwaangazia, ili waweze kusafiri mchana au usiku.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Wakati wa mchana bwana aliwatangulia kwa nguzo ya wingu kuwaongoza katika njia yao, na wakati wa usiku aliwatangulia kwa nguzo ya moto kuwaangazia, ili waweze kusafiri mchana au usiku.

Tazama sura Nakili




Kutoka 13:21
21 Marejeleo ya Msalaba  

Zaidi ya hayo ukawaongoza kwa nguzo ya wingu mchana; na kwa nguzo ya moto usiku; ili kuwapa mwanga katika njia iliyowapasa kuiendea.


hata hivyo wewe kwa wingi wa rehema zako hukuwaacha jangwani; nguzo ya wingu haikuondoka kwao wakati wa mchana, ili kuwaongoza njiani; wala nguzo ya moto haikuondoka wakati wa usiku, ili kuwapa mwanga na kuwaonesha njia watakayoiendea.


Alitandaza wingu liwe kifuniko, Na moto ili uwaangazie usiku.


Ee Mungu, ulipowaongoza watu wako, Ulipopita nyikani,


Uliwaongoza watu wako kama kundi, Kwa mkono wa Musa na Haruni.


Akawaongoza kwa wingu mchana, Na usiku kucha kwa nuru ya moto.


Akasema nao katika nguzo ya wingu. Wakashika shuhuda zake na amri aliyowapa.


Lakini akawaambia, Ehe, BWANA na awe pamoja nanyi, kama nitakavyowapa ruhusa kwenda zenu pamoja na watoto wenu; angalieni, kwa kuwa pana uovu huko mbele yenu.


Ilikuwa Haruni aliponena na huo mkutano wote wa wana wa Israeli, wakaangalia upande wa bara, na tazama, utukufu wa BWANA ukaonekana katika hilo wingu.


Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.


Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Mfano wake ni nguzo za moshi; Afukizwa manemane na ubani, Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?


Na wingu la BWANA lilikuwa juu yao mchana hapo waliposafiri kwenda mbele kutoka kambini.


kisha watawaambia wenyeji wa nchi hii; wamesikia wao ya kuwa wewe BWANA u kati ya watu hawa; maana, wewe BWANA waonekana uso kwa uso, na wingu lako lasimama juu yao, kisha wewe watangulia mbele yao, katika nguzo ya wingu mchana, na katika nguzo ya moto usiku.


aliyewatangulia njiani, usiku kwa moto, kuwaonesha njia mtakayoiendea, na mchana kwa hilo wingu, ili apate kuwatafutia mahali pa kusimamisha hema zenu.


Naye BWANA, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo