Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 12:50 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

50 Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli wote; kama BWANA alivyowaagiza Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

50 Waisraeli wote walitii sheria hiyo na kufanya kama Mwenyezi-Mungu alivyowaagiza Mose na Aroni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

50 Waisraeli wote walitii sheria hiyo na kufanya kama Mwenyezi-Mungu alivyowaagiza Mose na Aroni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

50 Waisraeli wote walitii sheria hiyo na kufanya kama Mwenyezi-Mungu alivyowaagiza Mose na Aroni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

50 Waisraeli wote walifanya kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa na Haruni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

50 Waisraeli wote walifanya kama vile bwana alivyomwagiza Musa na Haruni.

Tazama sura Nakili




Kutoka 12:50
21 Marejeleo ya Msalaba  

Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, majeshi yote ya BWANA yalitoka nchi ya Misri.


Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu, na kwa mgeni akaaye kati yenu ugenini.


Ilikuwa siku ile ile moja, BWANA akawatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri kwa majeshi yao.


Hawa ni Haruni yeye yule, na Musa yeye yule, BWANA aliowaambia, akisema, Watoeni wana wa Israeli watoke nchi ya Misri sawasawa na majeshi yao.


Lakini Farao hatawasikiza ninyi, nami nitaweka mkono wangu juu ya Misri, na kuyatoa majeshi yangu, watu wangu, hao wana wa Israeli, watoke nchi ya Misri kwa hukumu zilizo kuu.


kisha hizo fedha za ukombozi Musa akampa Haruni na wanawe, kama neno la BWANA, kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Basi hao binti za Selofehadi wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa;


Wana wa Israeli wakafanya hivyo, wakawatoa na kuwaweka nje ya kambi; kama BWANA alivyonena na Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.


Nami nimempa Haruni hao Walawi wawe kipawa chake yeye na wanawe, kutoka kwa wana wa Israeli, ili wafanye kazi ya kutumikia wana wa Israeli katika hema ya kukutania, kisha wafanye upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli; ili kusiwe na maradhi kati ya wana wa Israeli, hapo wana wa Israeli watakapopakaribia mahali patakatifu.


Basi Musa na Haruni, na mkutano wote wa wana wa Israeli, wakawafanyia Walawi mambo hayo; kama hayo yote BWANA aliyomwagiza Musa kwa habari za hao Walawi, ndivyo wana wa Israeli walivyowafanyia.


Kisha baada ya hayo Walawi wakaingia ili wafanye kazi zao ndani ya hema ya kukutania mbele ya Haruni na mbele ya wanawe; kama BWANA alivyomwagiza Musa kuhusu hao Walawi, ndivyo walivyowafanyia.


Nao wakaiadhmisha Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika bara ya Sinai vile vile kama hayo yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.


na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.


Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.


Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.


Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia, fanyeni.


Neno lolote ninalowaagiza lizingatieni, usilizidishe, wala usilipunguze.


Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.


Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo