Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 12:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 “Mwezi huu utakuwa kwenu mwezi wa kwanza wa mwaka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 “Mwezi huu utakuwa kwenu mwezi wa kwanza wa mwaka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 “Mwezi huu utakuwa kwenu mwezi wa kwanza wa mwaka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu, yaani mwezi wa kwanza wa mwaka wenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 “Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu, yaani mwezi wa kwanza wa mwaka wenu.

Tazama sura Nakili




Kutoka 12:2
14 Marejeleo ya Msalaba  

Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hadi mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari.


BWANA akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia,


Mwezi wa kwanza, siku ya mwezi kumi na nne, wakati wa jioni, mtakula mikate isiyochachwa, hata siku ya mwezi ishirini na moja jioni.


Waambieni mkutano wote, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;


Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa BWANA aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa.


Ninyi mwatoka leo katika mwezi wa Abibu.


Utaiweka sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu; utakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba kama nilivyokuagiza, kwa wakati uliowekwa, mwezi wa Abibu (kwa maana ndio mwezi uliotoka Misri); wala hapana mtu atakayeonekana mbele yangu na mikono mitupu;


Hiyo sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu utaitunza. Utakula mikate isiyotiwa chachu muda wa siku saba, kama nilivyokuagiza, kwa majira yaliyoaganwa katika mwezi wa Abibu; kwa kuwa ulitoka Misri katika mwezi huo wa Abibu.


Hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili, siku ya kwanza ya mwezi maskani ile ilisimamishwa.


Bwana MUNGU asema hivi; Mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, utatwaa ng'ombe dume mchanga na mkamilifu; nawe utapatakasa mahali patakatifu.


Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, mtakuwa na Pasaka, sikukuu ya siku saba; mkate usiotiwa chachu utaliwa.


Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa jioni, ni Pasaka ya BWANA.


Tena, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, ni Pasaka ya BWANA.


Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie Pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo