Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 11:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 na wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri watakufa, tangu yule mzaliwa wa kwanza wa Farao aketiye katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa huyo kijakazi aliye pale nyuma ya jiwe la kusagia; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Nitakapopita, kila mzaliwa wa kwanza nchini Misri atakufa: Kuanzia mzaliwa wa kwanza wako wewe Farao ambaye ni mrithi wako, hadi mzaliwa wa kwanza wa mjakazi anayesaga nafaka kwa jiwe. Hata wazaliwa wa kwanza wa mifugo nao wote watakufa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Nitakapopita, kila mzaliwa wa kwanza nchini Misri atakufa: Kuanzia mzaliwa wa kwanza wako wewe Farao ambaye ni mrithi wako, hadi mzaliwa wa kwanza wa mjakazi anayesaga nafaka kwa jiwe. Hata wazaliwa wa kwanza wa mifugo nao wote watakufa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Nitakapopita, kila mzaliwa wa kwanza nchini Misri atakufa: kuanzia mzaliwa wa kwanza wako wewe Farao ambaye ni mrithi wako, hadi mzaliwa wa kwanza wa mjakazi anayesaga nafaka kwa jiwe. Hata wazaliwa wa kwanza wa mifugo nao wote watakufa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kila mwanaume kifungua mimba katika Misri atakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Farao, anayeketi kwenye kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mjakazi, anayesaga nafaka kwa jiwe, pamoja na kila mzaliwa wa kwanza wa mifugo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kila mwanaume kifungua mimba katika Misri atakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Farao, aketiye penye kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mtumwa wa kike, anayesaga nafaka kwa jiwe, pamoja na kila mzaliwa wa kwanza wa mifugo.

Tazama sura Nakili




Kutoka 11:5
13 Marejeleo ya Msalaba  

Akawapiga wazaliwa wa kwanza katika nchi, Malimbuko ya nguvu zao.


Aliwapiga wazaliwa wa kwanza wa Misri, Wa wanadamu na wa wanyama.


Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wao wa kwanza; Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Akampiga kila mzaliwa wa kwanza wa Misri, Malimbuko ya nguvu katika hema za Hamu.


Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.


Hata ikawa, usiku wa manane BWANA akawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hadi mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.


basi ilikuwa hapo Farao alipojifanya kuwa mgumu ili asitupe ruhusa kuondoka, BWANA akawapiga wazaliwa wa kwanza wote waliokuwa katika nchi ya Misri, wa binadamu na wa mnyama; kwa ajili ya hayo namtolea BWANA wote wafunguao tumbo, wakiwa wa kiume; lakini wazaliwa wa kwanza wote wa wana wangu nawakomboa.


nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako.


Twaa mawe ya kusagia, usage unga; Vua utaji wako, ondoa mavazi yako, Funua mguu wako, pita katika mito ya maji.


Vijana huyachukua mawe ya kusagia; Na watoto hujikwaa chini ya kuni.


wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.


Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.


Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakateremka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo