Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 11:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Musa na Haruni walifanya ajabu hizo zote mbele ya Farao; BWANA akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, asiwape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Basi, Mose na Aroni walifanya maajabu hayo yote mbele ya Farao. Lakini Mwenyezi-Mungu alimfanya Farao kuwa mkaidi, akakataa kuwaruhusu Waisraeli waondoke nchini mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Basi, Mose na Aroni walifanya maajabu hayo yote mbele ya Farao. Lakini Mwenyezi-Mungu alimfanya Farao kuwa mkaidi, akakataa kuwaruhusu Waisraeli waondoke nchini mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Basi, Mose na Aroni walifanya maajabu hayo yote mbele ya Farao. Lakini Mwenyezi-Mungu alimfanya Farao kuwa mkaidi, akakataa kuwaruhusu Waisraeli waondoke nchini mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Musa na Haruni wakafanya maajabu haya yote mbele ya Farao, lakini Mwenyezi Mungu akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waondoke katika nchi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Musa na Haruni wakafanya maajabu haya yote mbele ya Farao, lakini bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waondoke katika nchi yake.

Tazama sura Nakili




Kutoka 11:10
17 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?


Lakini BWANA akaufanya ule moyo wa Farao uwe mgumu, asiwape wana wa Israeli ruhusa waende zao.


Lakini BWANA akaufanya kuwa mgumu moyo wa Farao, asikubali kuwapa ruhusa waende zao.


BWANA akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia,


Nami najua ya kuwa huyo mfalme wa Misri hatawapa ruhusa mwende zenu, la, hata kwa mkono wa nguvu.


BWANA akamwambia Musa, Hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizozitia mkononi mwako; lakini nitaufanya mgumu moyo wake, naye hatawapa ruhusa hao watu waende zao.


Nami nitaufanya mgumu moyo wa Farao, nami nitazifanya kuwa nyingi ishara zangu na ajabu zangu katika nchi ya Misri.


BWANA akaufanya mgumu moyo wa Farao, asiwasikize; vile vile kama BWANA alivyomwambia Musa.


Ee BWANA, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanya kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, makabila ya urithi wako.


Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.


Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.


Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyokuwa karibu kuharibiwa;


Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni hakutuacha kupitia kwake; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, alifanya roho yake kuwa ngumu, akamtia ukaidi moyoni mwake, apate kumtia mkononi mwako kama alivyo hivi leo.


Kwa kuwa lilikuwa ni la BWANA kuifanya mioyo yao kuwa migumu, hata wakatoka kupigana na Israeli, ili apate kuwaangamiza kabisa, wasihurumiwe lakini apate kuwaangamiza, kama vile BWANA alivyomwamuru Musa.


Mbona, basi, mnaifanya mioyo yenu migumu, kama vile wale Wamisri, na yule Farao, walivyoifanya mioyo yao migumu? Hata na hao, baada ya kuwadhihaki, je! Hawakuwaruhusu watu waende, nao wakaondoka?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo