Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 9:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Na wakati alipowatuma BWANA kutoka Kadesh-barnea, akiwaambia, Kweeni mkaimiliki nchi niliyowapa; ndipo mkaasi juu ya maagizo ya BWANA, Mungu wenu, hamkumsadiki wala hamkusikiza sauti yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Na Mwenyezi-Mungu alipowatuma kutoka Kadesh-barnea akisema, ‘Nendeni mkaimiliki nchi ambayo nimewapatia,’ mlimwasi; hamkusadiki wala hamkutii yale aliyowaambia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Na Mwenyezi-Mungu alipowatuma kutoka Kadesh-barnea akisema, ‘Nendeni mkaimiliki nchi ambayo nimewapatia,’ mlimwasi; hamkusadiki wala hamkutii yale aliyowaambia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Na Mwenyezi-Mungu alipowatuma kutoka Kadesh-barnea akisema, ‘Nendeni mkaimiliki nchi ambayo nimewapatia,’ mlimwasi; hamkusadiki wala hamkutii yale aliyowaambia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Vilevile wakati Mwenyezi Mungu alipowatuma kutoka Kadesh-Barnea, alisema, “Kweeni, mkaimiliki nchi niliyowapa.” Lakini mliasi dhidi ya agizo la Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Hamkumtegemea wala kumtii.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Vilevile wakati bwana alipowatuma kutoka Kadesh-Barnea, alisema, “Kweeni, mkaimiliki nchi ambayo nimewapa.” Lakini mliasi dhidi ya agizo la bwana Mwenyezi Mungu wenu. Hamkumtegemea wala kumtii.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 9:23
13 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa hawakumwamini Mungu, Wala hawakuutumainia wokovu wake.


Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.


Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,


Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule.


Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili.


Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; kinga iliyokuwa juu yao imeondolewa, naye BWANA yuko pamoja nasi; msiwaogope.


Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka Horebu kwa njia ya mlima wa Seiri mpaka Kadesh-barnea.


Akasema, Nitawaficha uso wangu, Nitaona mwisho wao utakuwaje; Maana, ni kizazi cha ukaidi mwingi, Watoto wasio imani ndani yao.


Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa Habari Njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo