Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 8:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo BWANA, Mungu wako, akurudivyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Kumbukeni kwamba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawarudi kama vile baba amrudivyo mwanawe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Kumbukeni kwamba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawarudi kama vile baba amrudivyo mwanawe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Kumbukeni kwamba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawarudi kama vile baba amrudivyo mwanawe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Mjue basi ndani ya mioyo yenu kama mtu anavyomwadibisha mwanawe, ndivyo Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atawaadibisha ninyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Mjue basi ndani ya mioyo yenu kama mtu anavyomwadibisha mwanawe, ndivyo bwana Mwenyezi Mungu wako atawaadibisha ninyi.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 8:5
19 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu;


Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo, Na uovu wao kwa mapigo.


Ee BWANA, heri mtu yule umwadibuye, Na kumfundisha kwa sheria yako;


Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.


Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na BWANA, Wala usione ni taabu kurudiwa naye.


Kwa kuwa BWANA ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye.


Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lolote litakalofuata baada yake.


Ng'ombe amjua bwana wake, Na punda ajua kibanda cha bwana wake; Bali Israeli hajui, watu wangu hawafikiri.


Basi, mwanadamu, funga tayari vyombo kwa uhamisho, ukahame wakati wa mchana mbele ya macho yao; nawe utahama toka mahali pako hapa mpaka mahali pengine mbele ya macho yao; labda watafahamu, wajapokuwa ni nyumba iliyoasi.


Kwa sababu atafakari, na kughairi, na kuyaacha makosa yake yote aliyoyatenda, hakika ataishi, hatakufa.


Ila tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia.


na huko jangwani, ulipoona alivyokuchukua BWANA, Mungu wako, kama mtu amchukuavyo mwanawe, njia yote mliyoiendea, hata mkafika mahali hapa.


Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la BWANA, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu chochote ulichokatazwa na BWANA, Mungu wenu,


Kutoka mbinguni amekufanya usikie sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake kutoka katika moto.


Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;


Nawe uzishike amri za BWANA, Mungu wako, upate kwenda katika njia zake, na kumcha.


Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo