Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 7:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Ila BWANA, Mungu wako, atawatoa mbele yako, atawatia mashaka, mashaka makuu, hata waishe kuangamizwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawatia adui zenu mikononi mwenu na atawafanya wahangaike mpaka waangamie.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawatia adui zenu mikononi mwenu na atawafanya wahangaike mpaka waangamie.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawatia adui zenu mikononi mwenu na atawafanya wahangaike mpaka waangamie.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Lakini Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atawatia watu hao mikononi mwenu, akiwatia katika machafuko makubwa hadi waangamizwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Lakini bwana Mwenyezi Mungu wenu atawatia watu hao mikononi mwenu, akiwatia katika kuchanganyikiwa kukubwa mpaka wawe wameangamizwa.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 7:23
11 Marejeleo ya Msalaba  

Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuoneshe maungo yao.


Pigeni kelele za hofu; maana siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.


Na waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu.


Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama maangamizi yatokayo kwake aliye Mwenyezi.


Tena mkono wa BWANA ulikuwa juu yao ili kuwaangamiza, kuwatoa katika kambi hadi walipouwawa.


Naye BWANA atawatia mikononi mwenu, nanyi mtawatenda kadiri ya amri ile niliyowaamuru.


Kama vile mataifa yale ambayo BWANA anawaangamiza mbele yenu, ndivyo mtakavyoangamia; kwa sababu hamkutaka kuisikiliza sauti ya BWANA, Mungu wenu.


Basi jua siku hii ya leo kuwa BWANA, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakapowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia BWANA.


watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;


BWANA naye akawatapanya mbele ya Israeli, naye Israeli akawaua uuaji ulio mkuu hapo Gibeoni, akawafukuza waikimbilie hiyo njia ya kukwelea kwenda Beth-horoni, na kuwapiga hadi kufikia Azeka, tena hadi kufikia Makeda.


BWANA akamfadhaisha Sisera na magari yake yote, na jeshi lake lote, kwa makali ya upanga, mbele ya Baraka; basi Sisera akashuka katika gari lake, akakimbia kwa miguu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo