Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 5:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu chochote alicho nacho jirani yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 “ ‘Usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba yake, wala shamba lake, wala mtumwa wake wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu chochote alicho nacho jirani yako.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 “ ‘Usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba yake, wala shamba lake, wala mtumwa wake wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu chochote alicho nacho jirani yako.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 “‘Usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba yake, wala shamba lake, wala mtumwa wake wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu chochote alicho nacho jirani yako.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ng’ombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ng’ombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.”

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 5:21
12 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari la jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.


Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke, Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu;


Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako.


Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake.


Nao hutamani mashamba, na kuyanyakua; na nyumba pia, nao huzichukua; nao humwonea mtu na nyumba yake, naam, mtu na urithi wake.


Ole wake yeye aipatiaye nyumba yake mapato mabaya, ili apate kukiweka kiota chake juu, apate kujiepusha na mkono wa uovu!


Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.


Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yoyote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.


Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo