Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 4:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yoyote siku ile BWANA aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 “Kwa hiyo muwe waangalifu msije kusahau kwamba: Mwenyezi-Mungu alipoongea nanyi kule mlimani Horebu katikati ya moto hamkumwona kwa umbo. Kwa sababu hiyo jihadharini sana,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 “Kwa hiyo muwe waangalifu msije kusahau kwamba: Mwenyezi-Mungu alipoongea nanyi kule mlimani Horebu katikati ya moto hamkumwona kwa umbo. Kwa sababu hiyo jihadharini sana,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 “Kwa hiyo muwe waangalifu msije kusahau kwamba: Mwenyezi-Mungu alipoongea nanyi kule mlimani Horebu katikati ya moto hamkumwona kwa umbo. Kwa sababu hiyo jihadharini sana,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Hamkuona umbo la aina yoyote siku ambayo Mwenyezi Mungu alizungumza nanyi kule Horebu kutoka kati ya moto. Kwa hiyo mjihadhari kwa uangalifu sana,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Hamkuona umbo la aina yoyote siku ambayo bwana alizungumza nanyi kule Horebu kutoka kwenye moto. Kwa hiyo mjihadhari kwa uangalifu sana,

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 4:15
22 Marejeleo ya Msalaba  

na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini BWANA hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu.


Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.


Mwezi wa tatu baada ya Waisraeli kutoka katika nchi ya Misri, siku iyo hiyo wakafika katika jangwa la Sinai.


Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.


Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.


Usigeuke kwa kulia wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni.


Basi, mtamlinganisha Mungu na nani? Au mtamfananisha na mfano wa namna gani?


BWANA asema hivi, Jihadharini nafsi zenu, msichukue mzigo wowote siku ya sabato, wala msiulete ndani kwa malango ya Yerusalemu;


Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzawa mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.


Naye akaandika juu ya mbao mfano wa maandiko ya kwanza, zile amri kumi, alizowaambia BWANA huko mlimani kutoka kati ya moto siku ya mkutano; BWANA akanipa.


BWANA akasema nanyi kutoka kati ya moto; mkasikia sauti ya maneno, lakini hamkuona umbo lolote; sauti tu.


BWANA akaniamuru wakati ule niwafundishe maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki.


Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la BWANA, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu chochote ulichokatazwa na BWANA, Mungu wenu,


Kutoka mbinguni amekufanya usikie sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake kutoka katika moto.


Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;


BWANA alisema nanyi uso kwa uso mlimani, kutoka kati ya moto;


Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi.


BWANA akanipa vile vimbao viwili vya mawe vilivyoandikwa kwa kidole cha Mungu; na juu yake yameandikwa maneno mfano wa yote aliyosema nanyi BWANA mle mlimani kutoka kati ya moto siku ya mkutano.


Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na chapa kamili ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi katika mkono wa kulia wa Ukuu huko juu;


Jihadharini nafsi zenu, basi, ili mmpende BWANA, Mungu wenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo