Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 32:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao, Alipowabagua wanadamu, Aliweka mipaka ya watu Kwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Mungu Mkuu alipoyagawia mataifa mali yao, alipowagawa wanadamu, kila taifa alilipatia mipaka yake,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Mungu Mkuu alipoyagawia mataifa mali yao, alipowagawa wanadamu, kila taifa alilipatia mipaka yake,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Mungu Mkuu alipoyagawia mataifa mali yao, alipowagawa wanadamu, kila taifa alilipatia mipaka yake,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Aliye Juu Sana alipowapa mataifa urithi wao, alipogawanya wanadamu wote, aliweka mipaka kwa ajili ya mataifa sawasawa na hesabu ya wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Aliye Juu Sana alipowapa mataifa urithi wao, alipogawanya wanadamu wote, aliweka mipaka kwa ajili ya mataifa sawasawa na hesabu ya wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 32:8
23 Marejeleo ya Msalaba  

Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,


Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye ni Yoktani.


Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.


Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Iwe urithi wenu mliopimiwa;


Waliopewa hiyo nchi peke yao, Wala mgeni hakupita kati yao);


Mbingu ni mbingu za BWANA, Bali nchi amewapa wanadamu.


Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.


Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la BWANA aliye juu.


Wewe uliiweka mipaka yote ya dunia, Majira ya joto na ya baridi wewe uliyafanya.


Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye Juu, enyi nyote.


Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.


Bali Wewe, BWANA, U Mtukufu hata milele.


Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye Juu.


Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye Juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.


Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye Juu alimpa Nebukadneza, baba yako, ufalme, na ukuu, na fahari, na utukufu;


Kwa hiyo hamtakuwa na mtu atakayeitupa kamba kwa kura katika mkutano wa BWANA.


Kutoka kilele cha majabali namwona; Na kutoka milimani namtazama; Angalia, ni watu wakaao peke yao, Wala hawatahesabiwa pamoja na mataifa.


Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Na kuyajua maarifa yake Aliye Juu. Yeye aonaye maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho,


Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;


Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizojengwa kwa mikono, kama vile asemavyo nabii,


Na Israeli anakaa salama, Chemchemi ya Yakobo peke yake, Katika nchi ya ngano na divai; Naam, mbingu zake zadondoza umande.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo