Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 32:50 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

50 ukafe katika kilima, huko ukweako, ukusanywe uwe pamoja na jamaa zako; kama alivyokufa nduguyo Haruni katika mlima wa Hori, akakusanywa awe pamoja na watu wake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

50 Kisha ufariki hukohuko mlimani kama kaka yako Aroni alivyofariki katika mlima Hori,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

50 Kisha ufariki hukohuko mlimani kama kaka yako Aroni alivyofariki katika mlima Hori,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

50 Kisha ufariki hukohuko mlimani kama kaka yako Aroni alivyofariki katika mlima Hori,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

50 Utafia kwenye mlima huo unaokwea na kukusanyika pamoja na watu wako, kama ndugu yako Haruni alivyofia juu ya Mlima Hori naye akakusanyika kwa watu wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

50 Utafia kwenye mlima huo unaokwea na kukusanyika pamoja na watu wako, kama ndugu yako Haruni alivyofia juu ya Mlima Hori naye akakusanyika kwa watu wake.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 32:50
12 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.


Ishmaeli aliishi miaka mia moja na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake.


Abrahamu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.


Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake.


Lakini nenda zako hata utakapokuwa mwisho ule; maana wewe utastarehe, nawe utaamka katika kura yako mwisho wa siku hizo.


na Nebo, na Baal-meoni, (majina yake yalikuwa yamegeuzwa) na Sibma; nao wakaiita miji waliyoijenga majina mengine.


Wakasafiri kutoka Hashmona, wakapiga kambi Moserothi.


Haruni akakwea mlima wa Hori, kwa amri ya BWANA, akafa hapo, katika mwaka wa arubaini baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, mwezi wa tano, siku ya kwanza ya mwezi.


BWANA akamwambia Musa, Tazama, siku zako za kufa zinakaribia, umwite Yoshua, nanyi mkajihudhurishe katika hema ya kukutania, ili nipate kumwagiza kazi. Musa na Yoshua wakaenda, wakajihudhurisha ndani ya hema ya kukutania.


BWANA akamwambia Musa, Angalia, wewe utalala na baba zako; na watu hawa wataondoka, wataifuata kwa ukahaba miungu ya kigeni ya nchi waiendeayo kuwa kati yao, nao wataniacha mimi na kulivunja agano langu, nililofanya nao.


Basi Musa, mtumishi wa BWANA, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo