Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 32:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

36 Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake, Atawahurumia watumwa wake, Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka, Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

36 Mwenyezi-Mungu atawatetea watu wake, na kuwahurumia watumishi wake, wakati atakapoona nguvu zao zimeishia, wala hakuna aliyebaki, mfungwa au mtu huru.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

36 Mwenyezi-Mungu atawatetea watu wake, na kuwahurumia watumishi wake, wakati atakapoona nguvu zao zimeishia, wala hakuna aliyebaki, mfungwa au mtu huru.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

36 Mwenyezi-Mungu atawatetea watu wake, na kuwahurumia watumishi wake, wakati atakapoona nguvu zao zimeishia, wala hakuna aliyebaki, mfungwa au mtu huru.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

36 Mwenyezi Mungu atawahukumu watu wake, na kuwahurumia watumishi wake atakapoona nguvu zao zimekwisha wala hakuna yeyote aliyebaki, mtumwa au aliye huru.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

36 bwana atawahukumu watu wake, na kuwahurumia watumishi wake atakapoona nguvu zao zimekwisha wala hakuna yeyote aliyebaki, mtumwa au aliye huru.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 32:36
24 Marejeleo ya Msalaba  

tazama, kwa hiyo mimi nitaleta mabaya juu ya nyumba yake Yeroboamu, nami nitakatilia mbali kutoka kwa Yeroboamu kila mwanamume, aliyefungwa na aliyeachwa katika Israeli, nami kuondoa nitawaondoa waliobaki wa nyumba yake Yeroboamu, kama mtu aondoavyo mavi, hata itakapokwisha pia.


Angalia, nitaleta mabaya juu yako; nami nitakuangamiza kabisa, nitamkatia Ahabu kila mwanamume, aliyefungwa na aliyeachwa katika Israeli.


Kwani BWANA akayaona mateso ya Israeli, kwamba yalikuwa machungu sana; maana hakukuwa na mfungwa wala asiyefungwa, wala msaidizi kwa ajili ya Israeli.


Kwa maana nyumba yote ya Ahabu wataangamia; nami nitamkatilia mbali kila mwanamume wa nyumba ya Ahabu, yeye aliyefungwa, na yeye asiyefungwa, katika Israeli.


Akawakumbukia agano lake; Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;


Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake, Na kuwahurumia watumishi wake.


Ataziita mbingu zilizo juu, Na nchi pia, ili awahukumu watu wake.


BWANA atawaamua mataifa, BWANA, unihukumu mimi, Kwa kadiri ya haki yangu, Kulingana na unyofu nilio nao.


Urudi, Ee BWANA utakasirika hadi lini? Wahurumie watumishi wako.


Mbele za BWANA, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake.


Na BWANA akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake.


Lakini BWANA yuko pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawatafaulu wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.


Je! Efraimu siye mwanangu mpendwa? Je! Siye mtoto apendezaye? Maana kila nisemapo neno juu yake, ningali nikimkumbuka sana; kwa sababu hiyo moyo wangu unataabika kwa ajili yake; bila shaka nitamrehemu, asema BWANA.


Ikiwa mtabaki katika nchi hii, ndipo nitawajenga, wala sitawabomoa, nami nitawapanda, wala sitawang'oa; kwa maana nayajutia mabaya niliyowatenda.


Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, hapo alipoinua mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni; akaapa kwa yeye aliye hai milele na milele, ya kwamba itakuwa nyakati tatu na nusu; tena watakapokuwa wamekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu, ndipo mambo hayo yote yatakapotimizwa.


Ni nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa BWANA, Mungu wenu?


Hapo ndipo BWANA alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake.


Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu wameyakataa maagizo yangu, na roho zao zimezichukia amri zangu.


BWANA akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema BWANA.


BWANA akaghairi katika jambo hili pia. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana MUNGU.


Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.


Na kila wakati BWANA alipowainulia waamuzi, ndipo BWANA alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana BWANA alisikitishwa na kilio chao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo