Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 32:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Isipokuwa niliogopa makamio ya adui, Adui zao wasije wakafikiri uongo, Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka, Wala BWANA hakuyafanya haya yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 ila tu kwa sababu ya majivuno ya maadui zao ili maadui zao wasije wakafikiria vingine; wasije wakasema, wamefaulu kuwaangamiza, nami Mwenyezi-Mungu sihusiki katika mambo haya!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 ila tu kwa sababu ya majivuno ya maadui zao ili maadui zao wasije wakafikiria vingine; wasije wakasema, wamefaulu kuwaangamiza, nami Mwenyezi-Mungu sihusiki katika mambo haya!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 ila tu kwa sababu ya majivuno ya maadui zao ili maadui zao wasije wakafikiria vingine; wasije wakasema, wamefaulu kuwaangamiza, nami Mwenyezi-Mungu sihusiki katika mambo haya!’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Lakini nilihofia dhihaka za adui, adui asije akashindwa kuelewa, na kusema, ‘Mikono yetu imeshinda; Mwenyezi Mungu hakufanya haya yote.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Lakini nilihofia dhihaka za adui, adui asije akashindwa kuelewa, na kusema, ‘Mikono yetu imeshinda; bwana hakufanya yote haya.’ ”

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 32:27
24 Marejeleo ya Msalaba  

Akaja yule mtu wa Mungu, akamwambia mfalme wa Israeli, akasema, BWANA asema hivi, Kwa sababu Washami wamesema, BWANA ni Mungu wa milima wala si Mungu wa nchi tambarare; basi nitawatia makutano haya yote walio wengi mkononi mwako, nanyi mtajua ya kuwa ndimi BWANA.


Ee BWANA, usimpe asiye haki tamaa zake, Usiifanikishe hila yake, wasije wakajiinua.


Nao wainuapo vichwa watu wanaonizunguka, Madhara ya midomo yao yawafunike.


Kwa nini Wamisri waseme, kuwa “Amewatoa ili awatende mabaya, apate kuwaua milimani na kuwaangamiza watoke juu ya uso wa nchi?” Geuza katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.


Mwambieni Hezekia, mfalme wa Yuda, maneno haya, mkisema, Asikudanganye Mungu wako unayemtumaini, akisema, Yerusalemu hautatiwa katika mikono ya mfalme wa Ashuru.


Nami nitaulinda mji huu, niuokoe kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.


Ukasema, Mimi nitakuwa malkia milele; hata hukuyatia hayo moyoni mwako, wala hukukumbuka mwisho wa mambo hayo.


Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu.


Kwa sababu wameniacha mimi, nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni, nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda; nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia;


Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, BWANA, mateso yangu; Maana huyo adui amejitukuza.


Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; uache dhambi zako kwa kutenda haki, uache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za fanaka.


Lakini mtu afanyaye neno lolote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana BWANA; na mtu huyo atatupiliwa mbali na watu wake.


isije nchi uliyotutoa ikasema, Ni kwa sababu BWANA hakuweza kuwaleta katika nchi aliyowahidi, tena ni kwa kuwa aliwachukia, aliwatoa nje ili kuwaua jangwani.


Maana Wakanaani na wenyeji wote wa nchi hii watasikia habari hii, nao watatuzingira, na kulifuta jina letu katika nchi. Nawe utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?


visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana BWANA hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza BWANA kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo