Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 32:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Hamkumjali Mwamba aliyewapa uhai, mlimsahau Mungu aliyewazaa nyinyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Hamkumjali Mwamba aliyewapa uhai, mlimsahau Mungu aliyewazaa nyinyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Hamkumjali Mwamba aliyewapa uhai, mlimsahau Mungu aliyewazaa nyinyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Mkamwacha Mwamba, aliyewazaa ninyi; mkamsahau Mungu aliyewazaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Mkamwacha Mwamba, aliyewazaa ninyi; mkamsahau Mungu aliyewazaa.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 32:18
19 Marejeleo ya Msalaba  

Wakamsahau Mungu, mwokozi wao, Aliyetenda makuu katika Misri.


BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.


Wadhalimu wataenda kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.


Maana umemsahau Mungu wa wokovu wako, wala hukuukumbuka mwamba wa ngome yako; kwa sababu hiyo ulipanda mashamba yapendezayo, na kutia ndani yake mizabibu migeni.


Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.


Ee kizazi litazameni neno la BWANA. Je! Nimekuwa jangwa kwa Israeli? Au nchi yenye giza kuu? Mbona watu wangu wanasema, Sisi tumetoroka, hatutaki kuja kwako tena?


Je! Mwanamwali aweza kusahau mapambo yake, au bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau mimi kwa muda wa siku zisizo na hesabu.


Sauti inasikiwa juu ya vilele vya milima, ni kulia kwao na maombi yao wana wa Israeli; kwa kuwa wameipotosha njia yao, wamemsahau BWANA, Mungu wao.


Ndani yako wamepokea rushwa ili kumwaga damu; umepokea riba na faida; nawe kwa choyo umepata mapato kwa kuwadhulumu jirani zako, nawe umenisahau mimi, asema Bwana MUNGU.


Maana Israeli amemsahau Muumba wake, naye amejenga nyumba za enzi; na Yuda ameongeza miji yenye maboma; lakini nitatuma moto juu ya miji yake, nao utaziteketeza ngome zake.


Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.


Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.


ndipo ujitunze, usije ukamsahau BWANA aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa.


Jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo.


basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau BWANA, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa;


Lakini itakuwa, kama ukimsahau BWANA, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawaonya leo ya kuwa mtaangamia bila shaka.


Lakini wakamsahau BWANA, Mungu wao, naye akawauza na kuwatia katika mikono ya Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori, na katika mikono ya Wafilisti, na katika mikono ya mfalme wa Moabu, nao wakapigana nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo