Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 32:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, Naye akala mazao ya mashamba; Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Aliwapitisha katika nyanda za juu za nchi, nao wakala mazao ya mashambani. Akawapa asali miambani waonje na mafuta kutoka mwamba mgumu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Aliwapitisha katika nyanda za juu za nchi, nao wakala mazao ya mashambani. Akawapa asali miambani waonje na mafuta kutoka mwamba mgumu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Aliwapitisha katika nyanda za juu za nchi, nao wakala mazao ya mashambani. Akawapa asali miambani waonje na mafuta kutoka mwamba mgumu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Akamfanya apande sehemu zilizoinuka za nchi, akamlisha kwa mavuno ya mashamba. Akamlea kwa asali toka mwambani, na kwa mafuta kutoka mwamba wa gumegume,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Akamfanya apande sehemu zilizoinuka za nchi, akamlisha kwa mavuno ya mashamba. Akamlea kwa asali toka mwambani, na kwa mafuta kutoka mwamba mgumu,

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 32:13
16 Marejeleo ya Msalaba  

Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu; Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.


Hataiangalia hiyo mito ya maji, Vile vijito vilivyojaa asali na siagi.


Wakati hatua zangu zilipokuwa zikioshwa kwa siagi, Nalo jabali liliponimiminia mito ya mafuta!


Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.


Naam, ningewalisha kwa ngano iliyo bora zaidi, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani.


Wala hawakuona kiu alipowaongoza jangwani; Alitoa maji katika mwamba kwa ajili yao; Pia akaupasua mwamba, maji yakatoka kwa nguvu.


ndipo utakapojifurahisha katika BWANA; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo.


Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikia hali ya kifalme.


Mimi nami nitapiga makofi, mimi nami nitashibisha ghadhabu yangu; mimi, BWANA, nimenena neno hili.


Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu adui amesema juu yenu, Aha! Na, Mahali pa juu pa zamani pamekuwa petu tupamiliki;


Kwa kadiri ya malisho yao, kwa kadiri iyo hiyo walishiba; walishiba na moyo wao ukatukuka; ndiyo sababu wamenisahau mimi.


kwa kuwa hukumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote;


Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake.


U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.


aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu,


nchi ya ngano na shayiri, na mizabibu, na mitini, na mikomamanga; nchi ya mizeituni yenye mafuta, na asali;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo