Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 31:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 na watoto wao wasiojua, wapate kusikia na kujifunza kumcha BWANA, Mungu wenu, siku zote mtakazokaa katika nchi mnayoivukia Yordani ili kuimiliki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Nao wazawa wao ambao hawajasikia sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, wapate kuisikia na kujifunza kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, muda wote mtakaoishi katika nchi ambayo mnakwenda kuimiliki ngambo ya mto Yordani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Nao wazawa wao ambao hawajasikia sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, wapate kuisikia na kujifunza kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, muda wote mtakaoishi katika nchi ambayo mnakwenda kuimiliki ngambo ya mto Yordani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Nao wazawa wao ambao hawajasikia sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, wapate kuisikia na kujifunza kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, muda wote mtakaoishi katika nchi ambayo mnakwenda kuimiliki ng'ambo ya mto Yordani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Watoto wao, ambao hawaijui sheria hii, lazima waisikie na kujifunza kumcha Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa muda mtakaoishi katika nchi mnayovuka Yordani kuimiliki.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Watoto wao, ambao hawaijui sheria hii, lazima waisikie na kujifunza kumcha bwana Mwenyezi Mungu wenu kwa muda mtakaoishi katika nchi mnayovuka Yordani kuimiliki.”

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 31:13
11 Marejeleo ya Msalaba  

Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.


ili vizazi vyenu vipate kujua ya kuwa niliwafanya wana wa Israeli kukaa katika vibanda, hapo nilipowaleta kutoka nchi ya Misri; mimi ndimi BWANA Mungu wenu.


Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hao watu wote waliokuwa wamebaki, wakaitii sauti ya BWANA, Mungu wao, na maneno ya nabii Hagai, kama BWANA, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za BWANA.


Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.


Nanyi leo jueni; kwa kuwa sisemi sasa na watoto wenu, ambao hawakujua, wala hawakuona adhabu ya BWANA, Mungu wenu, ukuu wake, na mkono wake wa nguvu, na mkono wake ulionyoka,


Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha BWANA, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii;


BWANA akamwambia Musa, Tazama, siku zako za kufa zinakaribia, umwite Yoshua, nanyi mkajihudhurishe katika hema ya kukutania, ili nipate kumwagiza kazi. Musa na Yoshua wakaenda, wakajihudhurisha ndani ya hema ya kukutania.


Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki.


siku ile uliyosimama mbele za BWANA wako huko Horebu, BWANA aliponiambia, Nikusanyieni watu hawa, nami nitawafanya wasikilize maneno yangu, ili wajifunze kunicha mimi siku zote watakazoishi duniani, wakapate na kuwafundisha watoto wao.


nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo