Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 30:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 mkimpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mkiitii sauti yake na kuambatana naye. Maana kufanya hivyo kunamaanisha kwamba mtapata maisha marefu na kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu aliwaahidi wazee wenu, Abrahamu, Isaka na Yakobo, kwamba atawapeni.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 mkimpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mkiitii sauti yake na kuambatana naye. Maana kufanya hivyo kunamaanisha kwamba mtapata maisha marefu na kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu aliwaahidi wazee wenu, Abrahamu, Isaka na Yakobo, kwamba atawapeni.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 mkimpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mkiitii sauti yake na kuambatana naye. Maana kufanya hivyo kunamaanisha kwamba mtapata maisha marefu na kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu aliwaahidi wazee wenu, Abrahamu, Isaka na Yakobo, kwamba atawapeni.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 na ili upate kumpenda Mwenyezi Mungu, Mungu wako, uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye uzima wako, na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi aliyoapa kuwapa baba zako Ibrahimu, Isaka na Yakobo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 na ili upate kumpenda bwana Mwenyezi Mungu wako, uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwa bwana ndiye uzima wako, na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi aliyoapa kuwapa baba zako Ibrahimu, Isaka na Yakobo.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 30:20
39 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.


Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.


BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?


Maana ghadhabu zake ni za muda mfupi tu; Radhi yake ni ya milele. Kilio huweza kuwapo usiku, Lakini furaha huja asubuhi.


Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima, Katika nuru yako tutaona nuru.


Umtumaini BWANA ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.


Aliyeiweka nafsi yetu katika uhai, Wala hakuuacha mguu wetu usogezwe.


Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na maagizo yangu yeyote atakayefanya hivyo ataishi; mimi ndimi BWANA.


Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.


Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


Naye, alipofika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa moyo wote.


wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu chochote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.


Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazawa wake.


Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkilishika lililo jema.


Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.


Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao.


Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;


Mche BWANA, Mungu wako, umtumikie yeye; ambatana naye, na kuapa kwa jina lake.


Kwa kuwa kama mtayazingatia kwa bidii maagizo haya yote niwaagizayo, kuyafanya; kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kutembea katika njia zake zote, na kushikamana naye;


nanyi mpate kuzifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, ya kuwa atawapa wao na kizazi chao, nchi imiminikayo maziwa na asali


Lakini mtakapovuka Yordani na kukaa katika nchi anayowarithisha BWANA, Mungu wenu, akawapeni raha, akiwaokoa na adui zenu pande zote, mkakaa salama;


kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda BWANA, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.


BWANA, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai.


Musa akaenda akawaambia Waisraeli maneno haya yote.


Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki.


Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu ninazowafundisha, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi anayowapa BWANA, Mungu wa baba zenu.


Bali ninyi mlioambatana na BWANA, Mungu wenu, mnaishi kila mmoja wenu, hata leo.


Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo BWANA, Mungu wako, milele.


Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili.


Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.


upate kumcha BWANA, Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezwe.


Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.


Jihadharini nafsi zenu, basi, ili mmpende BWANA, Mungu wenu.


bali shikamaneni na BWANA, Mungu wenu, kama mlivyotenda mpaka hivi leo.


Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye aliye na kiu, maji kutoka chemchemi ya maji ya uzima, bure.


Kisha akanionesha mto wa maji ya uzima, wenye kung'aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-kondoo,


Roho na Bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo