Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 30:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Lakini moyo wako ukikengeuka, usipotaka kusikiza, lakini ukavutwa kando kwenda kuabudu miungu mingine, na kuitumikia;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Lakini mkipotoshwa na kukataa kumsikiliza, mkavutwa kuabudu miungu mingine na kuitumikia,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Lakini mkipotoshwa na kukataa kumsikiliza, mkavutwa kuabudu miungu mingine na kuitumikia,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Lakini mkipotoshwa na kukataa kumsikiliza, mkavutwa kuabudu miungu mingine na kuitumikia,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Lakini kama moyo wako ukigeukia mbali ukawa huna utii, kama umevutwa kuisujudia miungu mingine na kuiabudu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Lakini kama moyo wako ukigeukia mbali ukawa huna utii, kama umevutwa kuisujudia miungu mingine na kuiabudu,

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 30:17
16 Marejeleo ya Msalaba  

na wa mataifa BWANA aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.


Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.


Ageukaye moyoni hushiba njia zake mwenyewe; Na mtu mwema ataridhika nafsini mwake.


Kwa kuwa mkigeuka msimfuate, yeye atawaacha tena nyikani; nanyi mtawaangamiza watu hawa wote.


Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kutumikia miungu mingine na kuiabudu;


Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno.


kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda BWANA, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.


nawahubiria hivi leo hakika mtaangamia; hamtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi, uivukiayo Yordani, uingie kuimiliki.


nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.


Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni;


Hadharini, ndugu zangu, usiwepo katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutoamini, ujitengao na Mungu aliye hai.


Nao wakawafikia hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakasema nao, wakinena,


Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu vya ubatili,


Lakini kama mkiendelea kutenda mabaya, mtaangamia, ninyi na mfalme wenu pia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo