Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Kumbukumbu la Torati 3:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Tukatwaa miji yake yote wakati huo; hapakuwa na mji tusiotwaa kwao miji sitini, nchi yote ya Argobu, ndio ufalme wa Ogu ulio katika Bashani.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Tuliiteka miji yake yote; hakuna hata mji mmoja ambao hatukuuteka. Jumla tuliiteka miji sitini, yaani eneo lote la Argobu ambalo lilitawaliwa na mfalme Ogu wa Bashani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Tuliiteka miji yake yote; hakuna hata mji mmoja ambao hatukuuteka. Jumla tuliiteka miji sitini, yaani eneo lote la Argobu ambalo lilitawaliwa na mfalme Ogu wa Bashani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Tuliiteka miji yake yote; hakuna hata mji mmoja ambao hatukuuteka. Jumla tuliiteka miji sitini, yaani eneo lote la Argobu ambalo lilitawaliwa na mfalme Ogu wa Bashani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Wakati huo tuliteka miji yake yote. Hakuna mji hata mmoja kati ya ile sitini ambao hatukuuteka, yaani eneo lote la Argobu, utawala wa Mfalme Ogu katika Bashani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Wakati huo tuliteka miji yake yote. Hakuna mji hata mmoja kati ya ile sitini ambao hatukuuteka, yaani eneo lote la Argobu, utawala wa Mfalme Ogu katika Bashani.

Tazama sura Nakili

Kumbukumbu la Torati 3:4
10 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana wa Geberi katika Ramoth-gileadi; na kwake ilikuwa miji ya Yairi mwana wa Manase iliyomo Gileadi; na kwake ilikuwa wilaya ya Argobu, iliyomo Bashani, miji mikubwa sitini yenye kuta na makomeo ya shaba.

Basi wakampiga, na wanawe, na watu wake wote, hata wasibakize kwake mtu yeyote; nao wakaimiliki nchi yake.

na nchi ya Gileadi iliyobaki, na Bashani yote, maana huo ufalme wa Ogu niliwapa nusu ya kabila la Manase; nchi yote ya Argobu, nayo ndiyo Bashani yote. (Na nchi hii yaitwa nchi ya Warefai.

Yairi, mwana wa Manase, alitwaa nchi yote ya Argobu, hata mpaka wa Wageshuri na Wamaaka; akaziita nchi hizo Hawoth-yairi, kwa jina lake mwenyewe, hata hivi leo, maana, hizo nchi za Bashani.)

Basi BWANA, Mungu wetu, akamtia mikononi mwako na Ogu mfalme wa Bashani, na watu wake wote; tukampiga, asibakizwe yeyote.

Miji hiyo yote ilikuwa yenye maboma marefu, na malango, na makomeo, pamoja na vijiji visivyokuwa na maboma, vingi sana.

wakaishika nchi yake, ikawa milki yao, na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, ndio wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki;

tena mpaka wa Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa wa hayo mabaki ya hao Warefai, aliyekaa Ashtarothi na Edrei,

Tufuate:

Matangazo

Matangazo