Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 3:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 hata BWANA awapumzishe ndugu zenu kama ninyi, nao pia waimiliki nchi wapewayo na BWANA, Mungu wenu, ng'ambo ya Yordani; ndipo mtakaporudi kila mmoja aende katika milki yake niliyowapa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Wasaidieni ndugu zenu Waisraeli mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowajalia watulie mahali pao kama nanyi mlivyotulia, yaani nao pia waimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapatia huko ngambo ya Yordani. Baada ya hayo, mtaweza kurejea katika nchi yenu hii ambayo nimewapeni iwe yenu!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Wasaidieni ndugu zenu Waisraeli mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowajalia watulie mahali pao kama nanyi mlivyotulia, yaani nao pia waimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapatia huko ngambo ya Yordani. Baada ya hayo, mtaweza kurejea katika nchi yenu hii ambayo nimewapeni iwe yenu!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Wasaidieni ndugu zenu Waisraeli mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowajalia watulie mahali pao kama nanyi mlivyotulia, yaani nao pia waimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapatia huko ng'ambo ya Yordani. Baada ya hayo, mtaweza kurejea katika nchi yenu hii ambayo nimewapeni iwe yenu!’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 hadi hapo Mwenyezi Mungu atakapowapa ndugu zenu kupumzika kama alivyowapa ninyi, wao pia wamiliki ile nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapa, ng’ambo ya Yordani. Baada ya hapo, kila mmoja wenu anaweza kurudi kwenye milki niliyowapa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 mpaka hapo bwana atakapowapa ndugu zenu kupumzika kama alivyowapa ninyi, wao pia wamiliki ile nchi ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa, ng’ambo ya Yordani. Baada ya hapo, kila mmoja wenu anaweza kurudi kwenye milki niliyowapa.”

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 3:20
9 Marejeleo ya Msalaba  

Sisi hatutarudia nyumba zetu, hata wana wa Israeli watakapokuwa wamekwisha kurithi kila mtu urithi wake.


na hiyo nchi kushindwa mbele za BWANA; ndipo baadaye mtarudi, nanyi mtakuwa hamna hatia mbele za BWANA, wala kwa Israeli; na nchi hii itakuwa milki yenu mbele za BWANA.


kwani hamjafikia bado katika raha na urithi akupao BWANA, Mungu wako.


Nikamwamuru Yoshua wakati huo, nikamwambia, Macho yako yameona yote aliyowatenda BWANA, Mungu wenu, wale wafalme wawili, navyo ndivyo atakavyoutenda BWANA kila ufalme huko uvukiako.


hadi BWANA atakapowapa ndugu zenu raha, kama alivyowapa ninyi, na wao pia wamepata kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu; ndipo mtakapoirudia nchi ya milki yenu na kuimiliki, ambayo Musa mtumishi wa BWANA aliwapeni ng'ambo ya Yordani upande wa maawio ya jua.


naye akawaambia, Ninyi mmeyafuata hayo yote mliyoamriwa na Musa, mtumishi wa BWANA, nanyi mmeisikia sauti yangu katika yote niliyowaamuru mimi;


Na sasa yeye BWANA, Mungu wenu, amewapa ndugu zenu kustarehe, kama alivyowaambia; basi sasa rudini ninyi mwende mahemani kwenu, hata nchi ya milki yenu, ambayo huyo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwapa ng'ambo ya pili ya Yordani.


kisha akanena nao, na kuwaambia, Rudini na mali mengi mahemani kwenu, na ng'ombe wengi sana, na fedha, na dhahabu, na shaba, na chuma, na mavazi mengi sana; mgawane na ndugu zenu hizo nyara za adui zenu.


Basi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase wakarudi, wakatoka kwa wana wa Israeli katika Shilo, ulioko nchi ya Kanaani, ili waende nchi ya Gileadi, hiyo nchi ya milki yao, waliyokuwa wanaimiliki, sawasawa na amri ya BWANA kwa mkono wa Musa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo