Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 3:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Nikawaamuru wakati huo, nikawaambia, BWANA, Mungu wenu, amewapa ninyi nchi hii muimiliki, basi vukeni ng'ambo wenye silaha mbele ya ndugu zenu, wana wa Israeli, nyote mlio mashujaa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 “Wakati ule niliwapa maagizo haya: ‘Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu amewapeni nchi hii mashariki ya mto Yordani iwe mali yenu. Sasa nyinyi mashujaa kati ya ndugu zenu, chukueni silaha mvuke mto Yordani mkiwa mbele ya ndugu zenu Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 “Wakati ule niliwapa maagizo haya: ‘Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu amewapeni nchi hii mashariki ya mto Yordani iwe mali yenu. Sasa nyinyi mashujaa kati ya ndugu zenu, chukueni silaha mvuke mto Yordani mkiwa mbele ya ndugu zenu Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 “Wakati ule niliwapa maagizo haya: ‘Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu amewapeni nchi hii mashariki ya mto Yordani iwe mali yenu. Sasa nyinyi mashujaa kati ya ndugu zenu, chukueni silaha mvuke mto Yordani mkiwa mbele ya ndugu zenu Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Wakati huo nilikuamuru: “Mwenyezi Mungu, Mungu wako, amekupa nchi hii uimiliki. Lakini ni lazima wanaume wenu wote wenye uwezo, wakiwa wamejiandaa tayari kwa vita, wavuke ng’ambo wakiwatangulia ndugu zako Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Wakati huo nilikuamuru: “bwana Mwenyezi Mungu wako amekupa nchi hii uimiliki. Lakini ni lazima wanaume wenu wote wenye uwezo, wakiwa wamejiandaa tayari kwa vita, wavuke ng’ambo wakiwatangulia ndugu zako Waisraeli.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 3:18
18 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha akamwambia, Mimi ni BWANA, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uimiliki.


Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele.


nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuishi humo; kwa kuwa mimi nimewapa ninyi hiyo nchi ili mwimiliki.


Hizi ndizo amri na hukumu mtakazofuataa kuzifanya katika nchi aliyokupa BWANA, Mungu wa baba zako, uimiliki, siku zote mtakazoishi juu ya nchi.


Lakini hawatakuwako maskini kwenu; (kwa kuwa BWANA atakubarikia kweli katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako;)


Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo BWANA, Mungu wako, uimiliki.


itenge miji mitatu iwe kwako katikati ya nchi yako, akupayo BWANA, Mungu wako, kuimiliki.


Kwa sababu hii ninakuamuru, na kukuambia, Ujitengee miji mitatu.


Aonekanapo mtu ameuawa katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, kuimiliki, amelala kondeni, wala haijulikani ni nani aliyempiga;


Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha BWANA, Mungu wako, katika adui zako wote walio kandokando, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.


Lakini wewe, simama hapa karibu nami, nami nitasema nawe sheria zote, na amri na hukumu, utakazowafunza, wapate kuzifanya katika nchi niwapayo kuimiliki.


Na hii ndiyo sheria, amri na hukumu, alizoziamuru BWANA, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayovuka kuimiliki;


Basi jua ya kuwa BWANA, Mungu wako, hakupi nchi hii nzuri uimiliki kwa ajili ya haki yako, kwa maana u taifa lenye shingo ngumu.


Piteni katika kambi, mkawaamuru hao watu, mkisema, Tayarisheni vyakula; kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, mpate kuimiliki.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo