Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 3:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Na nchi hiyo tuliitwaa ikawa milki yetu, wakati huo; kutoka Aroeri iliyo kwenye bonde la Arnoni, na nusu ya nchi ya milima ya Gileadi, na miji iliyokuwamo, niliwapa Wareubeni na Wagadi;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 “Tulipoitwaa nchi hiyo, niliwapa makabila ya Reubeni na Gadi eneo la kuanzia kaskazini mwa Aroeri karibu na Arnoni na nusu ya eneo la milima ya Gileadi, pamoja na miji yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 “Tulipoitwaa nchi hiyo, niliwapa makabila ya Reubeni na Gadi eneo la kuanzia kaskazini mwa Aroeri karibu na Arnoni na nusu ya eneo la milima ya Gileadi, pamoja na miji yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 “Tulipoitwaa nchi hiyo, niliwapa makabila ya Reubeni na Gadi eneo la kuanzia kaskazini mwa Aroeri karibu na Arnoni na nusu ya eneo la milima ya Gileadi, pamoja na miji yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Katika nchi tuliyoiteka wakati ule, niliwapa kabila la Reubeni na Gadi eneo lililoko kaskazini la Aroeri kando ya Bonde la Arnoni, na nusu ya eneo la nchi ya vilima ya Gileadi, pamoja na miji yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Katika nchi tuliyoiteka wakati ule, niliwapa kabila la Reubeni na Gadi eneo lililoko kaskazini la Aroeri kando ya Bonde la Arnoni, na nusu ya eneo la milima ya Gileadi, pamoja na miji yake.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 3:12
10 Marejeleo ya Msalaba  

kutoka Yordani upande wa mashariki, nchi yote ya Gileadi, na ya Wagadi, na Wareubeni, na Wamanase, kutoka Aroeri iliopo karibu na bonde la Arnoni, yaani, Gileadi, na Bashani.


Basi Musa akampa Makiri, mwana wa Manase, Gileadi, naye akakaa humo.


Kutoka Aroeri iliyo katika ukingo wa bonde la Arnoni, na huo mji ulio ndani ya bonde, mpaka kufika Gileadi, hapakuwa na mji uliokuwa na ngome ndefu ya kutushinda; BWANA, Mungu wetu, aliiweka wazi yote mbele yetu; ila nchi ya wana wa Amoni hukuisongelea;


Nanyi mlipokuja mahali hapa, walitutokea kupigana juu yetu Sihoni mfalme wa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, tukawapiga;


tukaitwaa nchi yao, nayo tukawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila la Manase, iwe urithi.


na nchi ya Gileadi iliyobaki, na Bashani yote, maana huo ufalme wa Ogu niliwapa nusu ya kabila la Manase; nchi yote ya Argobu, nayo ndiyo Bashani yote. (Na nchi hii yaitwa nchi ya Warefai.


toka Aroeri, iliyo juu ya ukingoni pa bonde la Arnoni, hadi mlima wa Sioni (nao ndio Hermoni),


Tufuate:

Matangazo


Matangazo