Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 29:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Shikeni basi maneno ya agano hili myafanye, ili mfanikiwe katika yote mfanyayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Kwa hiyo muwe waangalifu kushika maneno yote ya agano hili ili mpate kufanikiwa katika kazi zenu zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Kwa hiyo muwe waangalifu kushika maneno yote ya agano hili ili mpate kufanikiwa katika kazi zenu zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Kwa hiyo muwe waangalifu kushika maneno yote ya agano hili ili mpate kufanikiwa katika kazi zenu zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Zingatieni masharti ya agano hili, ili mweze kustawi katika kila kitu mnachofanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Fuateni kwa bidii masharti ya Agano hili, ili kwamba mweze kustawi katika kila kitu mnachofanya.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 29:9
19 Marejeleo ya Msalaba  

uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;


Wakasimama Yuda wote mbele za BWANA, pamoja na wadogo wao, na wake zao, na watoto wao.


Na katika kila kazi aliyoanza kwa utumishi wa nyumba ya Mungu, na kwa torati, na kwa amri, ili kumtafuta Mungu wake, aliifanya kwa moyo wake wote, akafanikiwa.


Njia zote za BWANA ni fadhili na kweli, Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.


Watauliza njia ya kwenda Sayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njooni ninyi, mjiunge na BWANA, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa.


Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.


Haya ndiyo maneno ya agano BWANA alilomwamuru Musa alifanye na wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, pamoja na agano alilofanya nao Horebu.


Leo mmesimama nyote mbele za BWANA, Mungu wenu; wakuu wenu, na makabila yenu, na wazee wenu, na maofisa wenu, wanaume wote wa Israeli,


Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha BWANA, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii;


Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili.


BWANA hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi sote tuliopo hapa, tu hai.


Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda kulingana na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kulia, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.


Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.


Yoshua akawakusanya makabila yote ya Israeli huko Shekemu, akawaita wazee wa Israeli, na wakuu wao, na waamuzi wao, na maofisa wao nao wakaja mbele za Mungu.


Hapakuwa na hata neno moja katika hayo aliyoamuru Musa, ambalo Yoshua hakulisoma mbele ya kusanyiko lote la Waisraeli, na mbele ya wanawake, na watoto, na wageni waliokaa nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo