Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 28:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 BWANA atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya BWANA, Mungu wako, na kutembea katika njia zake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 “Mwenyezi-Mungu atawafanyeni kuwa watu wake watakatifu kama alivyowaahidi, kama mkizitii amri zake yeye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kufuata njia zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 “Mwenyezi-Mungu atawafanyeni kuwa watu wake watakatifu kama alivyowaahidi, kama mkizitii amri zake yeye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kufuata njia zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 “Mwenyezi-Mungu atawafanyeni kuwa watu wake watakatifu kama alivyowaahidi, kama mkizitii amri zake yeye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kufuata njia zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Mwenyezi Mungu atakufanya kuwa taifa lake takatifu, kama alivyokuahidi kwa kiapo, ukishika maagizo ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na kwenda katika njia zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 bwana atakufanya kuwa taifa lake takatifu, kama alivyokuahidi kwa kiapo, kama ukishika maagizo ya bwana Mwenyezi Mungu wako na kwenda katika njia zake.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 28:9
17 Marejeleo ya Msalaba  

Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.


Naam, kuhusu Sayuni yatasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye Juu Atauimarisha.


akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.


nami nitawarejesha tena waamuzi wako kama walivyokuwa hapo kwanza, na washauri wako kama hapo mwanzo; baada ya hayo utaitwa, Mji wa haki, mji mwaminifu.


Nao watawaita, Watu watakatifu, Waliokombolewa na BWANA; Nawe utaitwa, Aliyetafutwa, Mji usioachwa.


ili nipate kukitimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi itiririkayo maziwa na asali, kama ilivyo hivi leo. Ndipo nikajibu, nikasema, Amina, Ee BWANA.


Kisishikamane na mkono wako kitu chochote katika kitu kilichoharimishwa; ili ageuke BWANA na ukali wa hasira zake akurehemu, akuonee huruma, na kukufanya kuwa wengi, kama alivyowaapia baba zako;


Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako; BWANA Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.


bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kukitimiza kiapo chake alichowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.


Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu.


ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawaimarisha, atawathibitisha, atawatia nguvu na kuwapa msingi imara.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo