Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 28:59 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

59 ndipo atakapofanya BWANA mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

59 basi, Mwenyezi-Mungu atawaleteeni nyinyi na wazawa wenu mateso yasiyo ya kawaida, mateso makali yasiyoponyeka na ya kudumu, na magonjwa makali ya kudumu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

59 basi, Mwenyezi-Mungu atawaleteeni nyinyi na wazawa wenu mateso yasiyo ya kawaida, mateso makali yasiyoponyeka na ya kudumu, na magonjwa makali ya kudumu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

59 basi, Mwenyezi-Mungu atawaleteeni nyinyi na wazawa wenu mateso yasiyo ya kawaida, mateso makali yasiyoponyeka na ya kudumu, na magonjwa makali ya kudumu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

59 Mwenyezi Mungu ataleta mapigo ya kutisha juu yako na kwa wazao wako, maafa makali na ya kudumu, magonjwa mazito na ya kudumu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

59 bwana ataleta mapigo ya kutisha juu yako na kwa wazao wako, maafa makali na ya kudumu, magonjwa mazito na ya kudumu.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 28:59
16 Marejeleo ya Msalaba  

Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia, Angalieni, mtazame Kama kuna majonzi yoyote mfano wa majonzi yangu, Niliyotendwa mimi, Ambayo BWANA amenihuzunisha kwa hayo Siku ya hasira yake iwakayo.


Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, BWANA, mateso yangu; Maana huyo adui amejitukuza.


Wafalme wa dunia hawakusadiki, Wala wote wakaao duniani, Ya kwamba mtesi na adui wangeingia Katika malango ya Yerusalemu.


Naye ameyathibitisha maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuzi wetu waliotuamua, kwa kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu.


Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago;


Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.


Kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hata sasa, wala haitakuwa kamwe.


nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu, na juu ya uzao wako milele;


Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, BWANA, MUNGU WAKO;


Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe.


Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata chini ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya milima.


Nilisema, Ningewatawanyia mbali, Ningekomesha kumbukumbu lao kati ya wanadamu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo