Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 28:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, kuongezeka kwa ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 “Mtabarikiwa mpate wazawa wengi, mavuno mengi, ng'ombe na kondoo wengi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 “Mtabarikiwa mpate wazawa wengi, mavuno mengi, ng'ombe na kondoo wengi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 “Mtabarikiwa mpate wazawa wengi, mavuno mengi, ng'ombe na kondoo wengi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na mifugo wako wachanga, yaani ndama wa makundi yako ya ng’ombe, na wana-kondoo wa makundi yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ng’ombe, na wana-kondoo wa makundi yako.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 28:4
16 Marejeleo ya Msalaba  

katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao;


Ikawa tokea wakati alipomweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, na vyote vilivyomo, BWANA akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Baraka za BWANA zikawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.


Naam, kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia; Kwa baraka za juu mbinguni. Baraka za vilindi vilivyo chini, Baraka za maziwa, na za mimba.


Naye aliwabariki wakaongezeka sana, Wala hawapunguzi mifugo wao.


Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA, Uzao wa tumbo ni thawabu.


Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Katika nyumba yako. Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.


Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo.


Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.


Mwenye haki aendaye katika unyofu wake, Watoto wake wabarikiwa baada yake.


Nami nitawaelekezea uso wangu, na kuwapa uzazi mwingi, na kuwaongeza; nami nitalithibitisha agano langu pamoja nanyi.


BWANA atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.


Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, kuongezeka kwa ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo wako.


Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.


Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.


naye atakupenda na kukubariki na kukuongeza tena ataubariki uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, kuongezeka kwa ng'ombe na kondoo wako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa.


Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo