Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 28:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

36 BWANA atakupeleka wewe, na mfalme wako utakayemweka juu yako, kwa taifa usilolijua wewe wala baba zako; nawe huko utatumikia miungu mingine ya miti na mawe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

36 “Mwenyezi-Mungu atawapeleka nyinyi na mfalme wenu mtakayejichagulia, mpaka kwa taifa ambalo nyinyi hamkulijua wala wazee wenu. Na huko mtatumikia miungu mingine ya miti na mawe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

36 “Mwenyezi-Mungu atawapeleka nyinyi na mfalme wenu mtakayejichagulia, mpaka kwa taifa ambalo nyinyi hamkulijua wala wazee wenu. Na huko mtatumikia miungu mingine ya miti na mawe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

36 “Mwenyezi-Mungu atawapeleka nyinyi na mfalme wenu mtakayejichagulia, mpaka kwa taifa ambalo nyinyi hamkulijua wala wazee wenu. Na huko mtatumikia miungu mingine ya miti na mawe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

36 Mwenyezi Mungu atakupeleka wewe na mfalme uliyemweka juu yako uende kwenye taifa ambalo hukulijua wewe wala baba zako. Huko utaabudu miungu mingine, miungu ya miti na mawe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

36 bwana atakupeleka wewe na mfalme uliyemweka juu yako uende kwenye taifa ambalo hukulijua wewe wala baba zako. Huko utaabudu miungu mingine, miungu ya miti na mawe.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 28:36
31 Marejeleo ya Msalaba  

Na mabaki ya watu waliosalia katika mji, nao wale walioasi, na kumkimbilia mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu wote wengine, watu hao Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawachukua mateka.


Naye mfalme wa Babeli akawapiga, na kuwaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Hivyo Yuda wakachukuliwa utumwani kutoka nchi yao.


Kwa hiyo BWANA akaleta juu yao makamanda wa jeshi la mfalme wa Ashuru, waliomkamata Manase kwa minyororo, wakamfunga kwa pingu, wakamchukua mpaka Babeli.


Watu wa nchi wakamtwaa Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtawaza awe mfalme katika Yerusalemu mahali pa babaye.


Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mnyonge; akawatia wote mkononi mwake.


Na wale waliookoka na upanga akawachukua mpaka Babeli; wakamtumikia yeye na wanawe hata kulipoingia milki ya Uajemi;


Juu yake akakwea Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akamfunga kwa pingu, amchukue mpaka Babeli.


Na baadhi ya wana wako utakaowazaa, watakaotoka kwako, watawachukulia mbali; nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli.


Nami nitakulazimisha kuwatumikia adui zako katika nchi usiyoijua; maana moto umewashwa katika hasira yangu, utakaowateketeza ninyi.


basi, kwa sababu hiyo, nitawatoeni katika nchi hii, na kuwaingiza katika nchi ambayo hamkuijua, wala ninyi wala baba zenu; na huko mtawatumikia miungu mingine mchana na usiku; kwa maana mimi sitawapa fadhili zangu hata kidogo.


Hata ikawa, Yerusalemu ulipotwaliwa, (katika mwaka wa tisa wa Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na jeshi lake lote, wakaja juu ya Yerusalemu, wakauzingira;


Basi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa, nami nitawapa maji yenye sumu wayanywe.


Malango yake yamezama katika nchi; Ameyaharibu makomeo yake na kuyavunja; Mfalme wake na wakuu wake wanakaa Kati ya mataifa wasio na sheria; Naam, manabii wake hawapati maono Yatokayo kwa BWANA.


Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao; Ambaye kwa habari zake tulisema, Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa.


Nami nitawatoa ninyi nje kutoka katikati yake, na kuwatia katika mikono ya wageni, nami nitafanya hukumu kati yenu.


Na katika habari zenu, enyi nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi, Nendeni, mkavitumikie vinyago vyenu kila mmoja wenu; na wakati wa baadaye pia, kama hamtaki kunisikiliza; lakini jina langu takatifu hamtalitia unajisi tena, kwa matoleo yenu, na kwa vinyago wenu.


BWANA atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe.


nanyi mliona machukizo yao, na sanamu zao, miti na mawe, fedha na dhahabu, zilizokuwako kwao;)


Na BWANA atawatawanya kati ya mataifa, nanyi mtasalia watu wachache kati ya makabila, mtakakopelekwa mbali na BWANA.


Na huko mtatumikia miungu, waliotengenezwa kwa mikono ya watu, miti na mawe, miungu ambao hawaoni, hawasikii, hawali, wala hawanusi.


Lakini kama mkiendelea kutenda mabaya, mtaangamia, ninyi na mfalme wenu pia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo