Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 28:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 utakwenda kwa kupapasapapasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Mtakwenda kwa kupapasapapasa mchana kama vipofu wala hamtafanikiwa katika shughuli zenu. Mtakuwa mkidhulumiwa kila mara na hakutakuwa na mtu wa kuwasaidieni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Mtakwenda kwa kupapasapapasa mchana kama vipofu wala hamtafanikiwa katika shughuli zenu. Mtakuwa mkidhulumiwa kila mara na hakutakuwa na mtu wa kuwasaidieni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Mtakwenda kwa kupapasapapasa mchana kama vipofu wala hamtafanikiwa katika shughuli zenu. Mtakuwa mkidhulumiwa kila mara na hakutakuwa na mtu wa kuwasaidieni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Adhuhuri utapapasapapasa kama kipofu gizani. Hutafanikiwa katika lolote ufanyalo; siku baada ya siku utadhulumiwa na kunyang’anywa, wala hakuna yeyote atakayekuokoa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Wakati wa adhuhuri utapapasapapasa huku na huko kama mtu kipofu katika giza. Hutafanikiwa katika lolote ufanyalo; siku baada ya siku utaonewa na kunyang’anywa, wala hakuna yeyote atakayekuokoa.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 28:29
26 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakashindwa kuupata mlango.


Nayo yawapatia faida nyingi wafalme uliowaweka kututawala kwa sababu ya dhambi zetu; tena wana mamlaka juu ya miili yetu, na juu ya wanyama wetu, kadiri wapendavyo, nasi tuko katika dhiki kuu.


Wao hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga, Naye huwafanya kupepesuka kama mlevi.


Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vile vile kama usiku.


BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako kuelekea mbinguni, kuwe giza juu ya nchi ya Misri, watu wapapasepapase gizani.


Twapapasapapasa kutafuta ukuta kama kipofu, naam, twapapasa kama watu wasio na macho; twajikwaa wakati wa adhuhuri, kana kwamba ni wakati wa ukungu wa alfajiri; kati yao walionenepa tumekuwa kama wafu.


Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu.


Hutangatanga njiani kama vipofu, Wametiwa unajisi kwa damu; Hata ikawa hakuna aliyeweza Kuyagusa mavazi yao.


Kwa sababu hiyo mioyo yetu imezimia; Kwa ajili ya hayo macho yetu hayaoni vema.


Watumwa wanatutawala; Hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao.


Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.


Wachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati.


Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.


BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;


Nao wakawasumbua na kuwaonea wana wa Israeli mwaka huo; waliwaonea wana wa Israeli wote waliokuwa ng'ambo ya pili ya Yordani katika nchi ya Waamori, iliyoko huko Gileadi, muda wa miaka kumi na minane.


Wana wa Israeli wakafanya tena yaliyo mabaya mbele za macho ya BWANA, BWANA akawatia katika mikono ya Wafilisti, muda wa miaka arubaini.


Wana wa Israeli walimtumikia Egloni mfalme wa Moabu muda wa miaka kumi na minane.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo