Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 28:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Mwenyezi-Mungu atawapiga kwa majipu yaliyowapata Wamisri, atawapeni vidonda, upele na kuwashwa ambavyo hamwezi kuponywa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Mwenyezi-Mungu atawapiga kwa majipu yaliyowapata Wamisri, atawapeni vidonda, upele na kuwashwa ambavyo hamwezi kuponywa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Mwenyezi-Mungu atawapiga kwa majipu yaliyowapata Wamisri, atawapeni vidonda, upele na kuwashwa ambavyo hamwezi kuponywa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Mwenyezi Mungu atakupiga kwa majipu ya Misri na kwa vidonda vinavyotoa usaha na kuwashwa, ambavyo huwezi kuponywa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 bwana atakupiga kwa majipu ya Misri na kwa vidonda vitokavyo usaha na kuwashwa, ambako huwezi kuponywa.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 28:27
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akawapiga watesi wake akawarudisha nyuma, Akawatia aibu ya milele.


akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.


Basi wakatwaa majivu ya tanuri, na kusimama mbele ya Farao; na Musa akayarusha juu mbinguni nayo yakawa ni majipu yenye kufura na kutumbuka juu ya wanadamu na juu ya wanyama.


Nao wale waganga hawakuweza kusimama mbele ya Musa kwa sababu ya hayo majipu, kwa maana hao waganga walikuwa na majipu, na Wamisri wote walikuwa nayo.


Nayo yatakuwa ni mavumbi membamba juu ya nchi yote ya Misri, nayo yatakuwa majipu yenye kufura na kutumbuka juu ya wanadamu na juu ya wanyama, katika nchi yote ya Misri.


Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na BWANA ataifunua aibu yao.


au aliye na kibyongo, au aliyedumaa, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu;


Nimewaletea tauni, kama tauni ya Misri; vijana wenu nimewaua kwa upanga, na farasi wenu nimewachukulia mbali; nami nimeupandisha uvundo wa kambi zenu na kuuingiza katika mianzi ya pua zenu; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.


BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;


BWANA atakupiga magoti na miguu kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa.


Na BWANA atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yoyote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao.


Na wale wasiokufa walipigwa kwa yale majipu; na kilio cha mji kikafika mbinguni.


Lakini mkono wa BWANA ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi, akawaangamiza, akawapiga kwa majipu, huko Ashdodi na mipakani mwake.


Ikawa, walipolihamisha, mkono wa BWANA ulikuwa juu ya mji huo, kwa kuwafadhaisha sana; akawapiga watu wa mjini, wadogo kwa wakubwa, wakapatwa na majipu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo