Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 28:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

26 Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Maiti zenu zitakuwa chakula cha ndege wala hapatakuwa na mtu atakayewafukuza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Maiti zenu zitakuwa chakula cha ndege wala hapatakuwa na mtu atakayewafukuza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Maiti zenu zitakuwa chakula cha ndege wala hapatakuwa na mtu atakayewafukuza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Mizoga yenu itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwa na mtu yeyote wa kuwafukuza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Mizoga yenu itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwepo mtu yeyote wa kuwafukuza.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 28:26
11 Marejeleo ya Msalaba  

Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila.


Watu wao waliouawa watatupwa nje, na uvundo wa maiti zao utapaa juu, na milima itayeyushwa kwa damu yao.


Nami nitaamrisha juu yao namna nne, asema BWANA; upanga uue, na mbwa wararue, na ndege wa angani, na wanyama wakali wa nchi, wale na kuangamiza.


watakufa kwa maradhi mabaya; hawataliliwa, wala hawatazikwa; watakuwa kama samadi juu ya uso wa nchi; nao wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa; na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi.


Nami nitalitangua shauri la Yuda na Yerusalemu mahali hapa; nami nitawaangusha kwa upanga mbele za adui zao, na kwa mkono wa watu watafutao roho zao; na mizoga yao nitawapa ndege wa angani na wanyama wakali wa nchi, iwe chakula chao.


mimi nitawatia katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao, na mizoga yao itakuwa ni chakula cha ndege wa mbinguni, na cha wanyama wakali wa nchi.


Na mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi; wala hapana mtu atakayewafukuza.


Wakati ule, asema BWANA, watatoa mifupa ya wafalme wa Yuda, na mifupa ya wakuu wake, na mifupa ya makuhani, na mifupa ya manabii na mifupa ya wenyeji wa Yerusalemu, itoke makaburini mwao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo