Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 28:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la BWANA, nao watakuwa na hofu kwako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Mataifa yote duniani yakiona kwamba nyinyi mnaitwa kwa jina la Mwenyezi-Mungu yatawaogopa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Mataifa yote duniani yakiona kwamba nyinyi mnaitwa kwa jina la Mwenyezi-Mungu yatawaogopa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Mataifa yote duniani yakiona kwamba nyinyi mnaitwa kwa jina la Mwenyezi-Mungu yatawaogopa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Kisha mataifa yote ya dunia wataona kuwa unaitwa kwa jina la Mwenyezi Mungu, nao watakuogopa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Kisha mataifa yote ya dunia wataona kuwa unaitwa kwa jina la bwana, nao watakuogopa.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 28:10
18 Marejeleo ya Msalaba  

Sifa za Daudi zikafika nchi zote; naye BWANA akawaletea mataifa yote hofu yake.


ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.


Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote.


Akayakwamisha magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa shida; na Wamisri wakasema, Na tuwakimbieni Waisraeli; kwa kuwa BWANA anawapigania.


Tumekuwa kama watu usiowamiliki kamwe; kama watu wasioitwa kwa Jina lako.


Kwa nini wewe umekuwa kama mtu aliyeshtuka, kama shujaa asiyeweza kuokoa? Lakini wewe, BWANA, u katikati yetu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache.


Na mji huu utakuwa kwangu jina la furaha, na sifa na utukufu, mbele ya mataifa yote ya dunia, watakaosikia habari ya mema yote niwatendeayo, nao wataogopa na kutetemeka, kwa sababu ya mema yote na amani nitakaoupatia mji huo.


Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.


Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabariki.


Ili wanadamu waliobakia wamtafute Bwana, Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao;


Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama mbele yenu; BWANA, Mungu wenu, ataweka utisho wenu na kuhofiwa kwenu juu ya nchi yote mtakayoikanyaga, kama alivyowaambia.


Hivi leo nitaanza mimi kutia utisho wako na kuhofiwa kwako juu ya watu walio chini ya mbingu kila mahali, watakaosikia uvumi wako, na kutetemeka, na kuingiwa na uchungu kwa sababu yako.


Ikawa, wafalme wa Waamori, waliokaa ng'ambo ya Yordani pande za magharibi, na wafalme wote wa Wakanaani, waliokuwa karibu na bahari, waliposikia jinsi BWANA alivyoyakausha maji ya Yordani mbele ya wana wa Israeli, hadi tulipokwisha kuvuka, basi mioyo yao iliyeyuka, wala haikuwamo roho ya nguvu ndani yao tena; kwa ajili ya wana wa Israeli.


Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo