Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 28:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 “Kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na kuzingatia kwa uangalifu amri ambazo ninawaamuru leo, yeye atawaweka juu ya mataifa yote duniani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 “Kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na kuzingatia kwa uangalifu amri ambazo ninawaamuru leo, yeye atawaweka juu ya mataifa yote duniani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 “Kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na kuzingatia kwa uangalifu amri ambazo ninawaamuru leo, yeye atawaweka juu ya mataifa yote duniani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ukimtii Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa ukamilifu na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa makini, Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kama ukimtii bwana Mwenyezi Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii, bwana Mwenyezi Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 28:1
31 Marejeleo ya Msalaba  

Daudi akajua ya kwamba BWANA amemweka imara ili atawale Israeli, na kwamba milki yake imetukuka zaidi kwa ajili ya watu wake Israeli.


Heri washikao hukumu, Na kutenda haki sikuzote.


Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri, Sifa zake zadumu milele.


Maana nayafuata mausia yako yote, kuwa ya adili, Kila njia ya uongo naichukia.


Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote.


Naye amewainulia watu wake pembe, Sifa za watauwa wake wote; Wana wa Israeli, watu walio karibu naye. Haleluya.


Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.


akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.


Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.


Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.


Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;


Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao


Niliyowaamuru baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika tanuri ya chuma, nikisema, Itiini sauti yangu, mkafanye sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu;


Kisha itakuwa, ikiwa watajifunza kwa bidii njia za watu wangu, kuapa kwa jina langu, Kama BWANA aishivyo, vile vile kama walivyowafundisha watu wangu kuapa kwa Baali, ndipo watakapojengwa kati ya watu wangu.


Na itakuwa, kama mkinisikiliza mimi kwa bidii, asema BWANA, msiingize mzigo wowote katika mlango wa mji huu siku ya sabato, bali muitakase siku ya sabato, bila kufanya kazi yoyote siku hiyo;


Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiishi katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.


Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.


akawaambia, Yeyote atakayempokea mtoto huyu kwa jina langu anipokea mimi; na yeyote atakayenipokea mimi ampokea yeye aliyenituma. Kwa kuwa aliye mdogo miongoni mwenu nyote huyo ndiye mkubwa.


Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.


wale ambao kwa subira katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoharibika, watapewa uzima wa milele;


Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati, ayafanye.


Tena itakuwa, mtakapoyazingatia kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote,


baraka ni hapo mtakapoyafuata maagizo ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizayo leo;


kwamba utaisikiza tu kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, uyatunze maagizo haya yote nikuagizayo leo, kuyafanya.


naye BWANA amekuungama hivi leo kuwa taifa iliyotengwa iwe yake yeye, kama alivyokuahidi, na kuwa yakupasa kushika maagizo yake yote;


na kuwa atakutukuza juu ya mataifa yote aliyoyafanya, kwa sifa, na jina, na heshima, nawe upate kuwa taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako, kama alivyosema.


BWANA atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo