Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 27:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 “ ‘Alaaniwe mtu yeyote anayepotosha haki ya mgeni au yatima au mjane’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 “ ‘Alaaniwe mtu yeyote anayepotosha haki ya mgeni au yatima au mjane’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 “‘Alaaniwe mtu yeyote anayepotosha haki ya mgeni au yatima au mjane’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 “Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 “Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 27:19
11 Marejeleo ya Msalaba  

Usiwafuate walio wengi kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;


Asiye haki hutoa rushwa kifuani, Ili kuzipotosha njia za hukumu.


Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.


Na mgeni akikaa pamoja nawe katika nchi yako, usimdhulumu.


Sikieni haya, tafadhali, enyi vichwa vya nyumba ya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli, mnaochukia hukumu, na kuipotosha adili.


Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami sitasita kutoa ushahidi juu ya wachawi; na juu ya wazinzi, na juu ya waapao kwa uongo; juu ya wamwoneao mwajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.


Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.


Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo