Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 25:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Kumbukeni walivyowashambulieni huko njiani mkiwa wanyonge na kuwapiga wale wote waliokuja nyuma yenu wamechoka. Waamaleki hawakumwogopa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Kumbukeni walivyowashambulieni huko njiani mkiwa wanyonge na kuwapiga wale wote waliokuja nyuma yenu wamechoka. Waamaleki hawakumwogopa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Kumbukeni walivyowashambulieni huko njiani mkiwa wanyonge na kuwapiga wale wote waliokuja nyuma yenu wamechoka. Waamaleki hawakumwogopa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Mlipokuwa mmechoka na kuishiwa nguvu kwa safari yenu, waliwalaki njiani, wakawapiga wale wote waliokuja nyuma. Waamaleki hawakumwogopa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Wakati mlipokuwa mmechoka na kuishiwa nguvu kwa safari yenu, wakawapiga wale wote waliokuja nyuma. Waamaleki hawakumwogopa Mungu.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 25:18
6 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini watawala wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arubaini za fedha; tena hata watumishi wao nao wakawatawala watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nilimcha Mungu.


Tena nilisema, Neno hili mnalolitenda si jema; je! Haiwapasi ninyi kwenda katika kicho cha Mungu wetu, kwa sababu ya mashutumu ya makafiri adui zetu?


Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.


Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.


Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu.


Kumcha Mungu hakupo machoni pao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo