Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 24:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili BWANA, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 “Mnapovuna mavuno yenu shambani na kusahau masuke mengine humo, msirudi kuyachukua, ila waachieni wageni, yatima na wajane, ili Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu awabariki katika kazi zenu zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 “Mnapovuna mavuno yenu shambani na kusahau masuke mengine humo, msirudi kuyachukua, ila waachieni wageni, yatima na wajane, ili Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu awabariki katika kazi zenu zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 “Mnapovuna mavuno yenu shambani na kusahau masuke mengine humo, msirudi kuyachukua, ila waachieni wageni, yatima na wajane, ili Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu awabariki katika kazi zenu zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Unapovuna shamba lako na ukasahau mganda, usirudi kuuchukua. Acha kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane, ili Mwenyezi Mungu, Mungu wako, aweze kukubariki wewe katika kazi zote za mikono yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Unapovuna shamba lako na ukasahau mganda, usirudi kuuchukua. Acha kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane, ili bwana Mwenyezi Mungu wako aweze kukubariki wewe katika kazi zote za mikono yako.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 24:19
23 Marejeleo ya Msalaba  

Basi hivyo BWANA akaubariki huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu moja, na punda wake elfu moja.


Ametoa kwa ukarimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.


Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri.


Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.


Bali muungwana huwaza mambo ya kiungwana, naye hushika sana mambo ya kiungwana.


Nanyi hapo mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala msiyakusanye masazo ya mavuno yako; utayaacha kwa ajili ya huyo maskini na mgeni; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.


Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.


Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.


na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.


Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia BWANA, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako.


bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, BWANA, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili.


nawe sema mbele ya BWANA, Mungu wako, Vitu vilivyo vitakatifu nimeviondoa katika nyumba yangu, nami mimewapa Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, kwa mfano wa maagizo yako uliyoniusia yote; sikukosa maagizo yako yoyote, wala sikuyasahau;


Tena mtoleeni kidogo katika matita na kukiacha, na akiokote, wala msimkataze.


Naye Ruthu Mmoabi akamwambia Naomi, Niruhusu niende shambani, niokote mabaki ya masuke nyuma yake yule ambaye nitaona kibali machoni pake. Akamwambia, Haya, mwanangu, nenda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo