Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 23:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Unapoweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, usichelewe kuitekeleza, maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wako ataidai kwako, nawe utakuwa na kosa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Unapoweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, usichelewe kuitekeleza, maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wako ataidai kwako, nawe utakuwa na kosa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Unapoweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, usichelewe kuitekeleza, maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wako ataidai kwako, nawe utakuwa na kosa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Ukiweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Ukiweka nadhiri kwa bwana Mwenyezi Mungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwa bwana Mwenyezi Mungu wako atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 23:21
24 Marejeleo ya Msalaba  

Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;


Utamwomba yeye naye atakusikia; Nawe utazitimiliza nadhiri zako.


Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA, Naam, mbele ya watu wake wote.


Asiyetoa fedha yake apate kula riba, Asiyepokea rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.


Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.


Ee Mungu, nadhiri zako ziko juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru.


Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.


Wekeni nadhiri na mziondoe Kwa BWANA, Mungu wenu. Wote wanaomzunguka wamletee hedaya, Yeye astahiliye kuogopwa.


na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.


ambaye hakumkopesha mtu ili apate faida, wala hakupokea ziada ya namna yoyote; naye ameuepusha mkono wake na uovu, na kufanya hukumu ya haki kati ya mtu na mwenzake;


Ndipo wale watu wakamwogopa BWANA mno, wakamtolea BWANA sadaka, na kuweka nadhiri.


Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa BWANA.


Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.


Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana viapo vyako;


na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.


Waweza kumtoza mgeni; lakini kila uwiacho kwa nduguyo mkono wako utamwachilia.


Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yoyote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili.


Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako.


Basi Yonathani akafanya agano na jamaa yake Daudi, akisema, BWANA na awalipize kisasi adui zake Daudi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo