Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 23:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Unaweza kutoza riba unapomkopesha mgeni, lakini ndugu yako Mwisraeli usimtoze riba, naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, atakubariki katika shughuli zako zote utakazofanya katika nchi ambayo unakwenda kuimiliki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Unaweza kutoza riba unapomkopesha mgeni, lakini ndugu yako Mwisraeli usimtoze riba, naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, atakubariki katika shughuli zako zote utakazofanya katika nchi ambayo unakwenda kuimiliki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Unaweza kutoza riba unapomkopesha mgeni, lakini ndugu yako Mwisraeli usimtoze riba, naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, atakubariki katika shughuli zako zote utakazofanya katika nchi ambayo unakwenda kuimiliki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili Mwenyezi Mungu, Mungu wako, akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoingia kuimiliki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili kwamba bwana Mwenyezi Mungu wako akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoingia kuimiliki.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 23:20
16 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo nikafanya shauri na nafsi yangu, nikagombana na wakuu na maofisa, nikawaambia, Nyote mnatoza watu riba, mtu na ndugu yake. Nikakutanisha mkutano mkubwa ili kukabiliana nao.


Asiyetoa fedha yake apate kula riba, Asiyepokea rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.


na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.


Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida.


Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.


Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;


Na itakuwa kama ilivyo hali ya watu, ndivyo itakavyokuwa hali ya kuhani; kama ilivyo hali ya mtumwa, ndivyo itakavyokuwa hali ya bwana wake; kama ilivyo hali ya mjakazi, ndivyo itakavyokuwa hali ya bibi yake; kama ilivyo hali yake anunuaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake auzaye; kama ilivyo hali yake akopeshaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake akopaye; kama ilivyo hali yake atwaaye faida, ndivyo itakavyokuwa hali yake ampaye faida.


ambaye hakumkopesha mtu ili apate faida, wala hakupokea ziada ya namna yoyote; naye ameuepusha mkono wake na uovu, na kufanya hukumu ya haki kati ya mtu na mwenzake;


Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe.


nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.


Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.


Msile nyamafu yoyote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.


Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia BWANA, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako.


Waweza kumtoza mgeni; lakini kila uwiacho kwa nduguyo mkono wako utamwachilia.


Atakufunulia BWANA hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo