Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 20:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo BWANA, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu chochote kipumzikacho;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Lakini katika miji ya nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapeni, msisalimishe chochote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Lakini katika miji ya nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapeni, msisalimishe chochote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Lakini katika miji ya nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapeni, msisalimishe chochote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Hata hivyo, katika miji ya mataifa ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapa kama urithi, msiache kitu chochote hai kinachopumua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Hata hivyo, katika miji ya mataifa ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa kama urithi, msiache kitu chochote hai kinachopumua.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 20:16
25 Marejeleo ya Msalaba  

Basi wakampiga, na wanawe, na watu wake wote, hata wasibakize kwake mtu yeyote; nao wakaimiliki nchi yake.


Basi kwa ajili hiyo mwueni kila mwanamume katika hao watoto, na kila mwanamke aliyemjua mwanamume kwa kulala pamoja naye.


ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunjavunja mahali pao pote palipoinuka;


Utaifanyia vivyo hivyo miji yote iliyo mbali sana nawe, isiyokuwa miji ya mataifa haya.


lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivyokuamuru BWANA, Mungu wako;


yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za BWANA; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi.


Naye BWANA atawatia mikononi mwenu, nanyi mtawatenda kadiri ya amri ile niliyowaamuru.


Tena BWANA alinikasirikia kwa ajili yenu, akaapa ya kwamba sitavuka Yordani, na ya kwamba sitaingia nchi ile njema, awapayo BWANA, Mungu wenu, iwe urithi.


Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa BWANA, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani jambo hilo litakuwa ni mtego kwako.


Kisha ikawa, hapo Yoshua, na wana wa Israeli, walipokuwa wamekwisha kuwaua watu wengi mno, hata wakaangamizwa, na hayo mabaki yao yaliyowasalia walipokuwa wamekwisha ingia katika miji yao yenye boma,


Siku hiyo Yoshua akautwaa mji wa Makeda, akaupiga kwa makali ya upanga, na mfalme wake; akawaangamiza kabisa na wote pia waliokuwamo ndani yake, hakumwacha hata mmoja aliyesalia; naye akamfanyia huyo mfalme wa Makeda kama alivyomfanyia huyo mfalme wa Yeriko.


Basi Yoshua akaipiga nchi hiyo yote, nchi ya vilima, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela, na nchi ya materemko, na wafalme wake wote; hakumwacha aliyesalia hata mmoja; lakini akawaharibu kabisa wote waliokuwa hai, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyoamuru.


Tena nyara zote za miji hiyo, na wanyama wa miji, wana wa Israeli walitwaa kuwa nyara zao wenyewe; lakini kila mtu wakampiga kwa makali ya upanga, hadi walipokuwa wamewaangamiza wote, wala hawakumsaza mmoja mwenye kuvuta pumzi.


Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake; bali fedha, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na vya chuma, wakavitia katika hazina ya nyumba ya BWANA.


Wote walioanguka siku hiyo wanaume kwa wanawake, walikuwa ni elfu kumi na mbili, yaani, watu wote wa mji wa Ai.


Kisha itakuwa, mtakapoushika mji, ndipo mtauteketeza mji kwa moto; sawasawa na hilo neno la BWANA; angalieni, nimewaagiza.


Nao wakamjibu Yoshua, na kusema, Ni kwa sababu ya sisi watumishi wako kuambiwa hakika, jinsi huyo BWANA, Mungu wako alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii yote, na kuwaangamiza wenyeji wote wa nchi hii watoke mbele zenu; kwa sababu hii tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, nasi tumefanya neno hili.


Siku iyo hiyo Yoshua akawafanya kuwa ni wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano, na kwa ajili ya madhabahu ya BWANA, hata siku hii ya leo, katika mahali hapo atakapopachagua.


Basi watu wa Israeli wakawaambia hao Wahivi, Labda mnakaa kati yetu; nasi tutawezaje kufanya agano nanyi?


Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo