Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 2:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 BWANA akaniambia, Usiwasumbue Wamoabi, wala usishindane nao katika mapigano; kwa kuwa sitakupa katika nchi yake kuimiliki; kwa sababu Ari nimewapa wana wa Lutu kuimiliki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Usiwasumbue watu wa Moabu, wala usipigane nao maana sitawapeni sehemu yoyote ya nchi yao. Ila eneo hilo la Ari nimewapa hao wazawa wa Loti liwe mali yao.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Usiwasumbue watu wa Moabu, wala usipigane nao maana sitawapeni sehemu yoyote ya nchi yao. Ila eneo hilo la Ari nimewapa hao wazawa wa Loti liwe mali yao.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Usiwasumbue watu wa Moabu, wala usipigane nao maana sitawapeni sehemu yoyote ya nchi yao. Ila eneo hilo la Ari nimewapa hao wazawa wa Loti liwe mali yao.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Kisha Mwenyezi Mungu akaniambia, “Usiwasumbue Wamoabu kwa vita, kwa kuwa sitawapa sehemu yoyote ya nchi yao. Nimetoa nchi ya Ari kwa wazao wa Lutu kama milki yao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Kisha bwana akaniambia, “Usiwasumbue Wamoabu kwa vita, kwa kuwa sitawapa sehemu yoyote ya nchi yao. Nimetoa nchi ya Ari kwa wazao wa Lutu kama milki yao.”

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 2:9
13 Marejeleo ya Msalaba  

Na sasa, tazama, wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, ambao hukuwaacha Israeli waingie katika nchi yao, walipotoka nchi ya Misri; lakini wakawageukia mbali, wasiwaharibu;


Ashuri naye amepatana nao, Wamewasaidia wana wa Lutu.


Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.


Na materemko ya hizo bonde Kwenye kuteremkia maskani ya Ari, Na kutegemea mpaka wa Moabu.


Maana, moto umetoka Heshboni, Umekuwa Ari ya Moabu, Mwali wa moto umetoka mji wa Sihoni; Wakuu wa mahali palipoinuka Arnoni.


Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile.


kama walivyonifanyia hao wana wa Esau waishio Seiri, na hao Wamoabi waishio Ari; hata nivuke Yordani niingie nchi tupewayo na BWANA, Mungu wetu.


msipigane nao; kwa kuwa sitawapa sehemu ya nchi yao kamwe, hata kiasi cha kukanyaga wayo wa mguu; kwa kuwa nimempa Esau milima ya Seiri kuwa milki yake.


akamwambia, Yeftha anakuambia hivi; Israeli hakuitwaa nchi ya Moabu, wala nchi ya wana wa Amoni;


ndipo Israeli wakatuma wajumbe waende kwa mfalme wa Edomu, wakisema, Nakuomba sana unipe ruhusa nipite katika nchi yako; lakini mfalme wa Edomu hangewasikiliza. Pia waliwatuma wajumbe kwa mfalme wa Moabu; wala naye hakukubali; basi Israeli wakakaa katika Kadeshi.


Kisha akaenda nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande wa mashariki mwa nchi ya Moabu, wakapiga kambi upande wa pili wa Arnoni; wala hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa Moabu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo