Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 2:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Tena mkono wa BWANA ulikuwa juu yao ili kuwaangamiza, kuwatoa katika kambi hadi walipouwawa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwakabili ili kuwaangamiza huko kambini, hata wote wakaisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwakabili ili kuwaangamiza huko kambini, hata wote wakaisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwakabili ili kuwaangamiza huko kambini, hata wote wakaisha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Mkono wa Mwenyezi Mungu uliwakabili hadi alipowaangamiza wote huko kambini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Mkono wa bwana uliwakabili hadi alipowaangamiza wote huko kambini.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 2:15
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo alipowainulia mkono wake na kuwaapia, Ya kuwa atawaangamiza jangwani,


Kwa maana mchana na usiku Mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.


Kwa hiyo akazikomesha siku zao kama pumzi, Na miaka yao kwa hofu ya kuwastusha.


Nanyi mtaona, na mioyo yenu itafurahi, na mifupa yenu itasitawi kama majani mabichi; na mkono wa BWANA utajulikana, uwaelekeao watumishi wake, naye atawaonea adui zake ghadhabu.


Waambieni, Kama niishivyo, asema BWANA, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi;


Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.


Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.


Kila walikokwenda mkono wa BWANA ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama BWANA alivyosema, na kama BWANA alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.


Kwa hiyo wakatuma watu waende kuwakusanya wakuu wote wa Wafilisti, wakasema, Liondoeni hilo sanduku la Mungu wa Israeli, liende tena mahali pake, ili lisituue sisi, wala watu wetu; kwa sababu kulikuwa na fadhaa kubwa sana mjini kote; mkono wa Mungu ulikuwa mzito mno huko.


Lakini mkono wa BWANA ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi, akawaangamiza, akawapiga kwa majipu, huko Ashdodi na mipakani mwake.


Ikawa, walipolihamisha, mkono wa BWANA ulikuwa juu ya mji huo, kwa kuwafadhaisha sana; akawapiga watu wa mjini, wadogo kwa wakubwa, wakapatwa na majipu.


Hivyo Wafilisti walishindwa, wasiingie tena ndani ya mipaka ya Israeli; na mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Wafilisti siku zote za Samweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo