Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 2:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Ndipo tukageuka, tukashika maisha ya jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu, kama alivyoniambia BWANA; tukaizunguka milima ya Seiri siku nyingi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 “Kisha, tuligeuka, tukasafiri jangwani kwa kupitia njia ya Bahari ya Shamu, kama Mwenyezi-Mungu alivyoniambia; tulitangatanga karibu na mlima Seiri kwa muda mrefu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 “Kisha, tuligeuka, tukasafiri jangwani kwa kupitia njia ya Bahari ya Shamu, kama Mwenyezi-Mungu alivyoniambia; tulitangatanga karibu na mlima Seiri kwa muda mrefu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 “Kisha, tuligeuka, tukasafiri jangwani kwa kupitia njia ya Bahari ya Shamu, kama Mwenyezi-Mungu alivyoniambia; tulitangatanga karibu na mlima Seiri kwa muda mrefu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kisha tukageuka nyuma na kusafiri kuelekea jangwani kwa njia inayoelekea Bahari ya Shamu, kama Mwenyezi Mungu alivyonielekeza. Kwa muda mrefu tulitembea kuzunguka nchi ya vilima ya Seiri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kisha tukageuka nyuma na kusafiri kuelekea jangwani kwa njia inayoelekea Bahari ya Shamu, kama bwana alivyonielekeza. Kwa muda mrefu tulitembea kuzunguka vilima katika nchi ya Seiri.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 2:1
7 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Mwamaleki na Mkanaani wakaa katika bonde; kesho geukeni, mkaende jangwani kwa njia iendayo Bahari ya Shamu.


Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia.


Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka Horebu kwa njia ya mlima wa Seiri mpaka Kadesh-barnea.


Na ninyi basi geukeni, mshike safari yenu, mwende jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu.


na alivyolifanya jeshi la Misri, farasi wao, na magari yao; na alivyowafunika kwa maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwaandama, na alivyowaangamiza BWANA hata hivi leo;


BWANA akasema, akaniambia,


Kisha akaenda nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande wa mashariki mwa nchi ya Moabu, wakapiga kambi upande wa pili wa Arnoni; wala hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa Moabu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo