Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 19:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 BWANA, Mungu wako, atakapoyakatilia mbali hayo mataifa yenye nchi akupayo BWANA, Mungu wako, nawe ukawafuata, na kukaa katika miji yao, na katika nyumba zao;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 “Baada ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuwaangamiza watu wale ambao nchi yao anawapeni, na baada ya kuimiliki na kuishi katika nyumba zao,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 “Baada ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuwaangamiza watu wale ambao nchi yao anawapeni, na baada ya kuimiliki na kuishi katika nyumba zao,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 “Baada ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuwaangamiza watu wale ambao nchi yao anawapeni, na baada ya kuimiliki na kuishi katika nyumba zao,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atakapokuwa amewaangamiza mataifa ambayo nchi yao anawapa ninyi, wakati mtakuwa mmewafukuza na kuishi katika miji yao na nyumba zao,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Wakati bwana Mwenyezi Mungu wenu atakapokuwa amewaangamiza mataifa ambayo nchi yao anawapa ninyi, wakati mtakapokuwa mmewafukuza na kuishi katika miji yao na nyumba zao,

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 19:1
11 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini kama hakumvizia, ila Mungu amemtia mkononi mwake; basi nitakuonesha mahali atakapopakimbilia.


Ndipo mtajiwekea miji itakayokuwa ya makimbilio kwa ajili yenu; ili kwamba mwenye kumwua mtu, pasipo kukusudia kumwua, apate kukimbilia huko.


Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,


Hizi ndizo amri na hukumu mtakazofuataa kuzifanya katika nchi aliyokupa BWANA, Mungu wa baba zako, uimiliki, siku zote mtakazoishi juu ya nchi.


BWANA, Mungu wako, atakapoyaondolea mbali hayo mataifa mbele yako, huko uingiako kuyamiliki, nawe ukawatwaa, na kuishi katika nchi yao;


Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, Nitaweka mfalme juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kandokando yangu;


Kisha BWANA Mungu wako atakapokuleta katika nchi aliyowaapia babu zako, Abrahamu na Isaka na Yakobo, ya kuwa atakupa; miji mikubwa mizuri usiyoijenga wewe,


na nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza wewe, na visima vilivyochimbwa usivyochimba wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba;


Kisha BWANA akanena na Yoshua, na kumwambia,


Nami nimewapa ninyi nchi msiyoitendea kazi, na miji msiyoijenga, nanyi mmekaa humo; mnakula matunda ya mashamba ya mizabibu na mizeituni msiyoipanda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo